Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS WAMETOA MAFUNZO YA UDHIBITI WA SUMUKUVU KWENYE MAHINDI NA KARANGA WILAYANI KONGWA


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel akifungua mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu kwenye mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake wilayani Kongwa Jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu kwenye mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake wilayani Kongwa wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.

*********************

Serikali kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imetoa mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu kwenye mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake chini ya Mradi wa Kitaifa wa Kudhibiti Sumukuvu "Tanzania Initiative for Preventing Aflatoxin Contamination - TANIPAC" wilayani Kongwa jijini Dodoma leo.

Akizungumza na washiriki wakati wa hafla ya ufunguzi wa mafunzo hayo wilayani hapa Mhe. Remidius Mwema Emmanuel alifarijika na mradi huo kutoa kipaumbele cha mafunzo kwa wilaya hiyo kwani elimu kuhusu sumukuvu inahitajika na ni matarajio yake kuwa italeta tija kwa biashara ya mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake .

Alifafanua kwamba anatambua nafasi ya wafanyabiashara, wasindikaji na wasafirishaji kwa ujumla wao na mchango walionao, hivyo ameishukuru serikali kwa kuandaa mafunzo hayo mahususi kwa ajili yao ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya udhibiti sumukuvu.

Alisisitiza umuhimu wa washiriki hao kuzingatia mafunzo hayo ili kuweza kuwa mabalozi wa elimu hiyo.

Akizungumzia na washiriki wilayani hapa kuhusu wilaya na mikoa itakayonufaika na mafunzo hayo Bw. Jabir Saleh Abdi mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu (TBS) alitaja wilaya nyingine zitakazonufaika na mafunzo haya ni za Kondoa, Chemba, Bahi, Kongwa, Babati, na Kiteto.

Wilaya zingine ni Namtumbo,Newala, Nanyumbu, Nzega, Urambo, Kibondo, Kasulu, Buchosa, Bukombe, Itilima, Kilosa na Gairo. Kuhusu mikoa zilizopo wilaya hizo, Abdi alisema ni Dodoma, Manyara, Ruvuma, Mtwara, Tabora, Kigoma, Mwanza, Geita, Simiyu na Morogoro

Abdi aliwataja walengwa wa mafunzo hayo kuwa ni wafanyabiashara, wasafirishaji na wasindikaji wa mahindi na karanga pamoja na bidhaa zake.

Tafiti za awali za mradi huu zimebaini maeneo hayo tajwa kuwa kuna changamoto ya uwepo wa sumukuvu katika mnyororo wa thamani wa mazao ya mahindi na karanga na bidhaa zake.

Post a Comment

0 Comments