Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania Mbunifu Majengo Daud Kondoro (Kulia,) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe (kushoto,) nakala ya taarifa za uhakiki ya wakazi 644 wa Magomeni kota katika mkutano maalumu uliowakutanisha na wakazi hao, leo jijini Dar ees Salaam.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe akizungumza katika mkutano huo uliowakutanisha na wakazi wa Magomeni kota na kueleza kuwa TBA ipo katika hatua za mwisho za umaliziaji na watahakikisha wakazi wote 644 wataingia katika makazi hayo, leo jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania Mbunifu Majengo Daud Kondoro akizungumza katika mkutano huo uliowakutanisha na wakazi wa Magomeni kota na kueleza kuwa TBA ipo katika hatua za mwisho za umaliziaji na watahakikisha wakazi wote 644 wataingia katika makazi hayo, leo jijini Dar es Salaam. Muonekano wa nyumba za makazi za Magomeni kota.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe (kulia,) akimkabidhi nakala ya uhakiki ya wakazi wa Magomeni kota Mwenyekiti wa Mtaa wa Magomeni George Abel (Kulia,) mara baada ya kutembelea makazi hayo na kuwataka wakazi hao kuyatunza kwa kiwango cha hali ya juu.
Sehemu ya wakazi wa Magomeni kota wakifuatilia mkutano uliowakutanisha na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, TAKUKURU na uongozi wa wakazi hao leo jijini Dar es Salaam.
************************************
WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA,) imekabidhi ripoti ya uhakiki wa wakazi 644 ambao wanatarajiwa kuishi katika makazi hayo kwa uongozi wa wakazi hao na kuwataka kushiriki katika kusahihisha dosari ambazo Wakala hiyo kwa kushirikiana na uongozi wa wakazi hao na Manispaa ya Kinondoni watahakikisha wanazitatua na wakazi wote 644 wanarejea katika makazi yao kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyoagiza.
Akisoma taarifa hiyo ya uhakiki katika mkutano uliowakutanisha na wakazi hao Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Mbunifu Majengo Daud Kondoro TBA amesema, wamepokea taarifa hiyo ya uhakiki kutoka kwa Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na kuwatambua wakazi 150 ambao wapo hai pamoja na wakazi 336 warithi wa wakazi halali wa makazi wakiwemo watoto, mke, mume au ndugu ambao wametambulika.
'' Kuna wakazi 98 ambao wana mikataba ya kuishi kwenye nyumba hizi ila majina yao hayafanani na yale yaliyowasilishwa katika uhakiki...tushirikiane katika kufanya masahisho na mapitio ili kuweka taarifa hizi sawa.'' Amesema.
Kondoro amesema, nyumba tisa na wakazi wake wametambulika kuwa wakazi wa makazi hayo ambao ni watumishi wa Serikali Ofisi ya Rais.
''Nyumba 44 zina ukinzani katika umiliki, taarifa imeonesha nyumba hizo zina mmiliki zaidi ya mmoja nawaomba tushirikiane katika hili kwa kutatua changamoto hii bila shida.'' Amesema Kondoro.
Aidha amesema wakazi saba kati ya 644 hawajapatikana kabisa na wakala hiyo kwa kushirikiana na Serikali na wakazi wa magomeni Kota wataangalia namna kuwatafuta wakazi hao waliosalia na kwa taarifa hiyo idadi ya wakazi wa nyumba hizo imebaki kama awali yaani 644.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Godwin Gondwe ameipongeza TBA kwa kusimamia vyema mradi huo na kuwaeleza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anatambua uhalali wao wa kuishi miaka mitano bure katika makazi hayo.
Gondwe amesema, hadi kufikia Januari mwakani wakazi hao watahamia katika nyumba hizo ambazo wameshazitembelea na kupewa semina elekezi ya namna ya kuishi na kutumia makazi hayo yaliyotolewa na TBA na kuwataka kutunza vyema miondombinu pamoja na kuzingatia usafi na usalama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Magomeni kota George Abel ameishukuru Serikali kwa kutimiza ahadi hiyo kwa kiwango cha juu na kuahidi kutatua chamhgamoto na migogoro kabla kuhamia katika makazi hayo ambayo watayatunza na kuyaenzi kama Serikali ya awamu ya tano iliyoongozwa na Hayati Dkt. John Josph Magufuli ilivyoahidi na kutekelezwa kwa kiwango cha juu na Serikali ya wamu ya sita.
0 Comments