*****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" imeshindwa kuendelea kwenye hatua inayofuata mara baada ya kushindwa kupata matokeo mazuri kwenye mechi za mwisho kwenye kundi lao.
Leo Taifa Stars imelazimishwa sare ya 1-1 na Madagascar kwenye mchezo wa mwisho hatua ya makundi kufuzu kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Taifa Stars ilianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Simon Msuva mnamo dakika ya 25 ya mchezo katika kipindi cha kwanza na kuiwezesha timu yake kuongoza katika kipindi chote cha kwanza.
kipindi cha pili timu ya Madagascar ilitawala mchezo ikihitaji kusawazisha goli kkatika mchezo huo kwani walifanya mabadiliko kadhaa ambayo kweli yaliza matunda japo Tanzania ilikuwa inacheza kwa kujihami.
Madagascar ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa nyota wao Hakim Abdalah na kuiwesha timu yake ya taifa kupata sare ya 1-1.
0 Comments