***************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Simba Sc imefanikiwa kuwachapa Red Arrows Fc ya nchini Zambia kwa mabao 3- katika mchezo ambao ulichezwa kwenye uwanjja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Licha ya uwanja kujaa maji Simba Sc ilicheza kandanda safi na kufanikiwa kuondoka mapumziko wakiwwa na faida ya mabao mawili yaliyofungwa na Benard Morrison pamoja na Meddie Kagere.
Kipindi cha pili kilianza Simba Sc ikionekana bado inahitaji magoli zaidi licha jya kuwa mbele kwa mabao mawili ambapo dakika 79 ilifanikiwa kupata bao la tatu kupitia tena kwa nyota wao Benard Morrison .
Simba inahitaji ushindi wowote ama sare katika mchezo ujao ili waweze kufuzu hatua ya makundi kombe la Shirikisho ambapo Red Arrows watakuwaa nyumbani kwenye mchezo huo.
0 Comments