Wanafunzi wakiwa kwenye sherehe za kilele cha Maadhimisho ya wiki ya msaada wa Sheria yaliyofanyika jana mkoani Singida kwa kuandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali la Sustanable Environment Management Action (SEMA) lenye makao yake makuu mkoani hapa kwa ufadhili wa Stromme Foundation East Africa.
Msajili Mkuu Msaidizi wa Asasi za Kiraia Mkoa wa Singida Patrick Kasango akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Kisheria mkoania Singida Pascal Tantau akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Maadhimisho yakiendelea.
Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirika la SEMA, Richard Temba akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Msaidizi wa kisheria kutoka Taasisi ya Wasaidizi wa Kisheria Mkoa wa Singida (WASS) Theddy Mande akitoa mada kwenye maadhimisho hayo.
Wakili wa Kujitegemea Lissa Abel akitoa mada kwenye maadhimisho hayo.
Picha ya pamoja.
Wasaidizi wa kisheria wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Maadhimisho yakiendelea.
************************
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHIRIKA lisilo la kiserikali la Sustanable Environment Management Action (SEMA) lenye makao yake makuu mkoani Singida limeadhimisha wiki ya msaada wa kisheria kwa kutoa elimu na msaada wa kisheria kwenye tasisi mbalimbali mkoani hapa ambapo kitaifa maadhimisho hayo yameafanyika mkoani Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika maadhimisho hayo Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Kisheria mkoania Singida Pascal Tantau alisema katika kuadhimisha siku hiyo wametoa elimu kwenye tasisi za kiselikari na binafsi na sehemu zenye watu wengi.
" Tumepata mafanikio makubwa katika wiki hii tumeweza kutatua changamoto nyingi za wananchi wenye matatizo ya kisheria kwa kushiriki mikutano ya hadhara iliyoandaliwa ngazi za kijamii, kutembelea Magereza mbalimbali na kuzungumza na mahabusu ili kujua changamoto zao za kisheria kwenye tuhuma zinazo wakabili pamoja na kushiriki katika vikao vya mahakama na kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi kwa kushirikiana na mashirika mengine kikiwepo Kituo cha Msaada wa Kisheria (LHRC).
Alisema changomoto kubwa walizokutana nazo ni za madai ya ardhi, mirathi ambazo wameweza kuzitafutia ufumbuzi na watu wamepata haki zao.
Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirika la SEMA, Richard Temba alisema wao kama wa wadau wakubwa wa haki wamefurahia sana kutoa elimu kwa watu mbalimbali hasa waliofika kwenye vituo au sehemu walizo zitenga kwa ajili ya kutolea elimu.
Alisema SEMA wana miradi ya Vijana kama Bonga ambao unawahusisha vijana kuanzia miaka 13-19 na mradi wa Tunaweza ambao ni wa vijana kuanzia miaka 20-35 na mradi wa Wekeza.
Temba alitumia nafasi hiyo kuelezea miradi mbalimbali ya vijana ya kuhimalisha uchumi inayofanywa na shirika hilo mkoani hapa ikiwepo ujenzi wa shule.
Alisema katika maadhimisho hayo yenye Kauli Mbiu isemayo 'Haki Jinai Inaweza Kupatikana kwa Wakati 'wameweza kutoa elimu ya kisheria ili vijana waweze kujua haki zao na kuacha kunyanyasika.
Katika maadhimisho hayo wasaidizi wa kisheria mkoani hapa waliweza kutoa mada mbalimbali kwa wananchi na wanafunzi.
Maadhmsho hayo yaliyokuwa na mafanikio makubwa yaliandaliwa na Shirika la SEMA kwa ufadhili wa Stromme Foundation East Africa.
0 Comments