Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAJIVUNIA MIAKA 60 YA UHURU KUONGEZA CHACHU KWA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt Dorothy Gwajima akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu changamoto na mafanikio ya Wizara katika miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara.

****************************

Na Mwandishi Wetu Dodoma



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt Dorothy Gwajima amesema Serikali imekua mstari wa mbele katika kuchochea ustawi na maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto kutoka Taifa lilivyopata uhuru mwaka 1961.

Akizungumza na waandishi wa habaril leo jijini Dodoma Dkt Gwajima amesema kwamba kupitia kampeni mbalimbali Serikali imeweza kujikita kuleta maendeleo ya Jamii kupitia kampeni mbalimbali kama kisomo chenye manufaa, Azimio la Arusha, Mtu ni Afya na kampeni ya Nyumba bora ambayo imewezasha nyumba 4008 kujengwa hadi sasa.

Dkt Gwajima ameongeza kuwa Serikali imepanua wigo wa kutoa mafunzo ya wataalam wa maendeleo ya jamii ambapo miaka ya 1960 kulikuwa chuo kimoja tu cha Tengeru na leo hii kuna jumla ya vyuo 63 ambapo, kati ya hivyo vya Serikali ni 12 na vya binafsi ni 51. Kati ya vyuo 12 vya Serikali 9 vinasimamiwa na Wizara ambapo mafunzo hayo yanatolewa kuanzia ngazi ya Astashahada hadi Shahada ya uzamili.

Dkt Gwajima amesema baada ya Uhuru Serikali imejielekeza kwenye kuimarisha Ustawi wa Watoto ambapo, katika miaka ya mwanzo ya 1970 Wizara ilikuwa inaratibu na kusimamia upatikanaji wa haki na ulinzi wa mtoto kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977. Ili kuimarisha upatikanaji wa haki, maendeleo na ustawi wa mtoto.

Waziri Dkt Gwajima ameongeza kuwa Wizara imeratibu uandaaji wa Programu Jumuishi ya Kitaifa ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (2021/22-2025/26) yenye lengo la kumlea na kumkuza mtoto kwa utimilifu wake. Katika kutimiza azma hiyo, Wizara imenzisha vituo vya kijamii 30 vya mfano ambapo lengo ni kujenga vituo hivyo katika Vijiji/Mtaa yote nchini.

Amesisitiza kuwa ushiriki wa Wazee katika masuala mbalimbali ya kijamii na kimaendeleo umeimarika baada ya Serikali kuweka utaratibu wa kuwa na Mabaraza ya Wazee katika ngazi zote, ambayo yameanzishwa kupitia Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003. Mabaraza 26 yameundwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara na kufanya Mabaraza kufikia 20,748.

Pia Waziri Dkt. Gwajima ameeleza kuwa kutokana na jitihada za uwezeshaji Wanawake hasa katika uongozi, kwa mara ya kwanza nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina Rais wa Awamu ya Sita ambaye ni mwanamke Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na pia amewahi kushika nyazifa mbalimbali kabla ya kuwa Rais. Wengine ni Mheshimiwa Anna Makinda, Spika wa Kwanza mwanamke wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Tulia Akson ambaye ni Naibu Spika wa sasa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dkt Gwajima amesisitiza kuwa Serikali imekuwa ikiratibu mashirika yasiyo ya kiserikali katika ngazi zote na katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru, Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa mashirika haya kwa kutunga Sheria Na. 24 ya mwaka 2002 ambayo ndiyo ilianza kuweka Taratibu za uratibu na usajili wa Mashirika hayo.

Aidha, ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru, Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa mashirika haya kwa kutunga Sheria Na. 24 ya mwaka 2002 ambayo ndiyo ilianza kuweka Taratibu za uratibu na usajili wa Mashirika hayo. Aidha, katika kuimarisha utoaji wa huduma za usajili na uratibu Serikali imefanikiwa kutengeneza Mfumo wa Kieletroniki wa Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NIS) kwa lengo la kuboresha mazingira ya utendaji kazi ili kuleta ufanisi na tija katika uratibu wa Mashirika hayo.

Post a Comment

0 Comments