


******************
Sekta zilizo chini ya Wizara ya Uwekezaji ikiwemo kituo cha Huduma za uwekezaji Nchini (TIC) imedhamiria kupunguza vikwazo wanavyokumbana navyo wawekezaji nchini ili kuongeza mapato yatakaenda kusaidia ujenzi wa miundombunu na kuboresha huduma kwa jamii ikiwa ni kuunga mkono dhamira Rais wa jamhuri a muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhakikisha anawaondolea kero wananchi wake
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Geoffrey Mwambe Akizungumza katika kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa mifumo na wadau mbalimbali katika sekta ya uwekezaji chenye lengo la kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wawekezaji hao, amesema Mamlaka zote na Taasisi zinashoghulikia wawekezaji kuweka mfumo mzuri ili kupunguza msululu upatikanaji wa leseni kwa wawekezaji hao.
Naye Mkurugenzi mtandaji wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Dkt Maduhu Kazi akaeleza namna mfumo huo utaweza kurahisisha kutoa huduma bora kwa wawekezaji.
0 Comments