******************
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera, amefungua mafunzo ya Wadau wa Sekta ya Usafirishaji kuhusu Sheria ya Afrika Mashariki ya Udhibiti Uzito wa Magari ya Mwaka 2016 na Kanuni zake za Mwaka 2018 yaliyoandaliwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).
Mafunzo hayo yamefunguliwa leo, Jumatatu Novemba mosi, 2021 jijini Mbeya, yakihudhuriwa na wadau kutoka Mikoa ya Songwe na Mbeya.
0 Comments