**************************
NA EMMANUEL MBATILO
Kiungo wa zamani Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Xavi Hernandez amejiunga rasmi na klabu hiyo kama kocha mkuu mara baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo Ronald Koeman.
Nyota huyo ambaye alicheza kwa mafanikio katika klabu hiyo ametambulishwa leo mbele ya waandishi wa habari na kupokelewa na mashabiki waliojitokeza kwenye dimba la Camp New.
Amesema amekuja katika klabu ambayo imemlea na kumtambulisha kwenye soka hivyo kuwa kocha katika klabu hiyo atahakikisha anapambana kurudisha mambo yalivyokuwa zamani.
0 Comments