Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS MHE.DKT. MWINYI ASHIRIKI MATEMBEZI YA KILOMITA 4 YA ZANZIBAR BLUE ECONOMY HAFL MARATHON 2021.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani kwa ajili ya kuaza kwa Mbio Zanzibar Blue Economoy Half Marathon 2021 za Kilomita 4 na kumalizia katika uwanja wa Amaan (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, wakijiandaa kuaza mbio hizo zilizofanyika leo 6-11-2021 ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Uongozi wake.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika matembezi ya Marathon ya Kilomita 4, yalioazia katika eneo la Mapinduzi Square Michezani na kumalizia katika Uwanja wa Amaan Zanzibar na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Mustafa Idrisa Kitwana na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, wakishiriki katika matembezi hayo ya Zanzibar Blue Economy Half Marathon 2021.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimvisha Nishani Mshindi wa kwanza wa Mbio za Kilomita 21 za Zanzibar Blue Economy Hafl Maradhon 2021 Francis Daman baada ya kubuka mshindi wa mbio hizo, zilizoazia katika eneo la Mapindizi Square Michezani na kumalizia Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia Wananchi wakati akiwa katika Matembezi ya Kilimota 4 ya Zanzibar Blue Economy Hafl Marathon 2021 yaliyoazia katika eneo la Mapinduzi Square Michezani Jijini Zanzibar na kumalizia katika Uwanja wa Amaan na (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi Maalum ya picha yake ya kuchora iliotolewa na Kamati ya Maandalizi ya Zanzibar Blue Ecenomy Hafla Marathon 2021 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg Abdalla Majura, baada ya kumaliza Matembezi ya Kilomita 4 ya Zanzibar Blue Economy Hafl Marathon 2021.(Picha na Ikulu)

WANANCHI wakiwa katika barabara ya Amani wakimshangilia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akipita katika eneo hilo wakati akiwa katika Matembezi ya Kilomita 4 ya Zanzibar Blue Economy Hafl Marathon, ikiwa ni Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Uongozi wake.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments