Mkutano Ukiendelea
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es salaam-UTAFITI Prof.Benadeta Killian akizungumza katika kikao ambacho kimewakutanisha wadau mbalimbali wa Utafiti masuala ya mabadiliko ya tabianchi kilichofanyika hapo jana katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Dkt.Zakia Abubakar akizungumza katika kikao ambacho kimewakutanisha wadau mbalimbali wa Utafiti masuala ya mabadiliko ya tabianchi kilichofanyika hapo jana katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mwakilishi wa Balozi wa Norway nchini Tanzania Bw.Ian Bryson akizungumza katika kikao ambacho kimewakutanisha wadau mbalimbali wa Utafiti masuala ya mabadiliko ya tabianchi kilichofanyika hapo jana katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Katika kuangalia mbinu zitakazosaidia Dunia kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya nchi, Serikali ya Norway kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wamezindua mradi unaolenga kufanyia utafiti mabadiliko ya tabia ya nchi, nishati na maendeleo endelevu hasa katika kipindi ambacho Dunia inapitia changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika kikao ambacho kimewakutanisha wadau mbalimbali wa Utafiti masuala ya mabadiliko ya tabianchi, Mhandisi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Pius Yanga amesema watajaribu kuangalia ni jinsi gani uwekezaji mkubwa katika gesi unaleta faida kwa wananchi wa kawaida ukiangalia hasa wale ambao wenye kipato kidogo na lipi lifanyike kuhakikisha kwamba wanaweza kufaidika zaidi.
Amesema katika uwekezaji huo pia unaweza kuleta athari mbalimbali hivyo wataangalia ni athari zipi zinaweza kujitokeza katika mazingira na kwa jamii husika na jinsi gani athari hizo tunaweza kuzikkabili.
"Matumaini yetu ni kwamba tunaweza kufanya utafiti ambao utatuletea matokeo mazuri. Huu mradi ni matokeo ya mradi mwingine wa miaka sita ambao umeisha mwaka jana na ule mradi tuumesomesha wanafunzi wa PHD 6, wanafunzi wa masters karibu sabini waliweza kupata ufadhiri asilimia 100 wakaeza kulipiwa na wote wakaingia masomoni". Amesema Mhandisi Yanda.
Amesema Mradi huo pia unanafasi ya kuweza kusomesha wanafunzi wa masters na PHD, wameshaanza mchakato wa kutangaza nafasi na tangazo la nafasi ya Masters limeshatoka na mtu ambaye atakuwa na hamasa ataweza kuomba hiyo nafasi basi yuko huru.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Balozi wa Norway nchini Tanzania Bw.Ian Bryson amesema katika mradi huo watakuwa wanaangalia zaidi mafuta na gesi katika maeneo ya Mtwara na Lindi na kuweza kuleta faida kwa wenyeji na wageni.
"Norway kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) tutajaribu kufanya utafiti uelewa zaidi kwa kushirikiana sana na wanakijiji pamoja na wakuu wa mikoa na wilaya kupeana mawazo kutokana na matokeo ya utafiti wetu na kujaribuu kuwashauri jinsi ya kujari haki za biinadamu ili ilete maendeleo ya maana". Amesema
0 Comments