Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kushoto akimkabidhi Mjasiriamali Rajab Msuya mkazi wa Tanga namba ya gari aina ya IST Mshindi wa shindano la Simbanking linaloendesha na benki ya CRDB hapa nchini mapema leo jijini Tanga kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa
Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa kushoto akimkabidhi Mjasiriamali Rajab Msuya mkazi wa Tanga funguo ya gari aina ya IST Mshindi wa shindano la Simbanking linaloendesha na benki ya CRDB hapa nchini mapema leo jijini Tanga kushoto ni Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa na kulia ni Meneja Mwandanizi wa Huduma Mbadala Benki hiyo Mangira Kibanda
Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mjasiriamali Rajab Msuya mkazi wa Tanga ambaye ni mshindi wa gari aina ya IST katika shindano la Simbanking linaloendesha na benki ya CRDB hapa nchini akielezea furaha yake.
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
MJASIRIAMALI Rajab Msuya mkazi wa Tanga amefanikiwa kuibuka mshindi wa gari aina ya IST katika shindano la Simbanking linaloendesha na benki ya CRDB hapa nchini
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa gari hiyo iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya CRDB tawi la Tanga iliyoshuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa pamoja na viongozi waandamizi wa benki hiyo kutoka Kanda pamoja na mkoani hapa.
Msuya alisema kuwa alishinda zawadi hiyo kutokana na kufanya miamala mbalimbali kupitia huduma hiyo ya Simbanking na hivyo kuweza kuibuka mshindi katika shindano la mwezi Septemba.
Alisema kwamba yeye alikuwa anafanya miamala minne kwa siku kutuma fedha ikiwemo kuhamisha kwenda akaunti yingine sanjari na malipo kupitia huduma mbalimbali ikiwemo kulipa bili kama vile za umeme na maji.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tanga Mgandilwa alisema kuwa serikali imekuwa ikihimiza matumizi ya teknolojia katika kufanya miamala mbalimbali ikiwemo huduma.
Alisema kuwa hivyo shindano hilo la CRDB inaonyesha ni namna gani ambavyo benki hiyo inaunga mkono jitihada za serikali katika kuongeza matumizi ya fedha kupitia huduma za mitandao.
Aidha alitoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutembea na fedha mifukoni badala yake wahakikishe wanaweka fedha zao banki ili waweze kuwa na uhakika wa usalama wa fedha zao ili kujiepusha dhidi ya watu wenye lengo la kuwaibia.
Kwa upande wake Meneja wa benki hiyo Kanda Kaskazini Chiku Isssa alisema kuwa maboresho ya huduma ya simbanking yameweza kulets mapinduzi makubwa ya huduma za kimtandao katika benki hiyo.
Alisema kuwa wameweza kufanikiwa kupunguza msongamano katika benki hiyo kutokana na kusogeza huduma zake karibu na wananchi .
Nae Meneja Mwandanizi wa Huduma Mbadala Benki hiyo Mangira Kibanda alisema kuwa huduma ya simbanking imeweza kusaidia kuongeza idadi ya wateja wanaotumia huduma hiyo.
Aliongeza kuwa matumizi ya miamala mbalimbali kupitia huduma hiyo imeweza kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 35% huku ya kutoa fedha imeweza kuongezeka kwa asilimia40%
0 Comments