*****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Mchezaji wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amefanikiwa kunyakua tuzo ya Ballon D'or kwa mwaka 2021 mbele ya mpinzani wake Robert Lewandowski ambaye ameibuka mshindi wa pili kwenye kinyang'anyiro hicho.
Wachezaji watano ambao waliiongia kwenye tano bora ni Lionel Messi(PSG), Ngolo Kante (Chelsea), Jorginho (Chelsea),Robert Lewandowski (Bayan Munich) na Karim Benzema (Real Madrid).
Messi amefanikiwa kuchukua tuzo hiyo mara saba kwake na kumuacha Christian Ronaldo ambaye amechukua tuzo hiyo mara tano.
Tuzo ya klabu bora ya mwaka imeenda kwa timu ya Chelsea ambayo imekjuwa na wachezaji wengi walioingia kwenye kinyang'anyiro ya tuzo ya Ballon D'OR.
Tuzo hizo zimetolewa leo usiku Novemba 29,2021 nchini Ufaransa.
0 Comments