Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary (katikati) akikata utepe wakati Shirika la Kivulini likikabidhi Pikipiki nne na Baiskeli 50 kwa ajili ya kusaidia kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto halmashauri ya Kishapu na Shinyanga.
******************************
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Kutetea haki za wanawake na Watoto -Kivulini limetoa msaada wa pikipiki 4 na Baiskel 50 zenye thamani ya shilingi milioni 27 kwa Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto, Idara za Maendeleo ya Jamii na vijiji 15 vya Halmashauri za Wilaya Shinyanga na Kishapu ili zisaidie utoaji wa elimu ya kuzuia na kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.
Lengo jingine ni kufanya ufuatiliaji wa mashauri ya mimba za utotoni, ndoa za utotoni na ukatili, ufuatiliaji wa shughuli za kamati za MTAKUWWA na wana mabadiliko 300 waliopo katika vijiji 15.
Hafla fupi ya makabidhiano ya pikipiki na baiskeli hizo imefanyika leo Alhamisi Novemba 4,2021 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary.
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally amesema wametoa pikipiki na baiskeli hizo ikiwa ni sehemu ya kufunga Mradi wa Kutokomeza Mimba za utotoni na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto unaotekelezwa na Kivulini kwa ufadhili wa OXFAM Tanzania ambao ulianza mwezi Septemba 2017 na kufungwa Oktoba 2021 katika kata 9 na vijiji 15 kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Kishapu.
“Tumekabidhi pikipiki nne zenye thamani ya shilingi Milioni 12 kwa ajili ya Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia na watoto halmashauri ya Kishapu na Shinyanga na Idara ya Maendeleo ya Jamii halmaashauri ya Kishapu na Shinyanga. Lakini pia tumekabidhi baiskeli 30 Kishapu na 20 Shinyanga kwa Maafisa Watendaji wa kata na vijiji na Wana Mabadiliko wa kujitolea ngazi ya jamii 300 kwa ajili kuongeza mapambano dhidi ya mimba na ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia”,amesema Ally.
Akifafanua zaidi, amesema pikipiki hizo zitatumiwa na Maafisa wa Madawati ya Jinsia na Watoto kutatua changamoto ya usafiri kwenda kutatua mashauri ya ubakaji,mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kwa upande wa Maafisa wa Idara za Maendeleo ya jamii watumie pikipiki hizo kwenda kwa jamii kutoa elimu ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Ameongeza kuwa baiskeli hizo zitatumiwa na Maafisa Watendaji wa kata na vijiji na Wana Mabadiliko wa kujitolea ngazi ya jamii kwa ajili ya kuifikia jamii kwa kutoa elimu na msaada kwa waathirika wa matukio ya ukatili wa kijinsia.
Amesema mradi huo uliofikia tamati, ulikuwa unahamasisha jamii kuzuia vitendo vyote vya ukatili kwa kuchukua hadharani bila uoga kuzuia matendo au dalili zozote za ukatili.
Ally amebainisha kuwa Mradi huo ulikuwa unatekelezwa katika kata tatu za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambazo ni Itwangi (vijiji vya Nduguti na Butini), Nsalala (Nsalala na Welezo) na Nyida kijiji cha Nyida.
Kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu kata 6 ambazo ni Uchunga (vijiji vya Kakola na Unyanyembe), Talaga (Nhobola), Ukenyenge (Bulimba na Negezi), Lagana (Mwamadulu na Lagana), Shagihilu (Shagihilu na Ndoleleji) na kata ya Kishapu kijiji cha Isoso.
Amezitaja baadhi ya changamoto walizokumbana nazo kuwa ni ukosefu wa usafiri kwa polisi kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa kata za mradi katika kutoa elimu na ufuatiliaji mashauri ya mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake ndiyo maana wameamua kutoa vifaa hivyo vya usafiri ili mapambano yaendelee.
Ameitaja changamoto nyingine kuwa Upelelezi wa mashauri ya mimba na ndoa za utotoni, ubakaji, ukatili dhidi ya wanawake na watoto kuchukua muda mrefu polisi bila kufikishwa mahakamani na waathirika wa matukio ya ukatili kutotoa ushahidi kwenye vyombo vya sheria.
Ally ameeleza kuwa, ili kufikia malengo yake na kupata matokeo tarajiwa katika mkoa wa Shinyanga, Kivulini imetekeleza shughuli mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia Septemba 2017 hadi Disemba 2021 katika kata 9 na vijiji 15 na kuwafikia umma wa watu 79949 (47155 wanawake, wanaume 32794) ambao wamekuwa wana mabadiliko wa kupinga na kuzuia vitendo vya ukatili kwa kuchukua hatua za kupinga vitendo hivyo.
“Kivulini imefanikiwa kujenga uwezo kwa umma wa watu 79949 wanaopinga na kuzuia ukatili katika jamii. Kupitia kamati za MTAKUWWA na Wana Mabadiliko ambao wapo katika ngazi ya kata,vijiji na vitongoji kwenye kata na vijiji vya mradi tumefanikiwa kutoa elimu ya masuala ya kuzuia ukatili dhidi ya wanawake na watoto,kuzuia mimba mashuleni, ndoa za utotoni,upakaji samba, utoro na kuongeza ufaulu shuleni”,ameeleza Ally.
“Pia tumehamasisha wanajamii kujenga nyumba bora kwa kutumia kipato kinachopatikana kupitia kilimo na ufugaji. Hali kadhalika Kivulini imefanikiwa kuzijengea uwezo kamati 9 za ulinzi wa wanawake na watoto wenye wajumbe 255. Kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya tumesaidia jamii kutambua umuhimu wa thamani ya elimu kwa mtoto wa kike”,amefafanua.
Akipokea pikipiki na baiskeli hizo, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary amelishukuru Shirika la Kivulini na Wafadhili shirika la OXFAM kwa kutoa msaada huo na kushirikiana na serikali katika kuleta mabadiliko chanya katika jamii ili kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
“Niwashukuru na kuwapongeza Kivulini kwa kuzijengea uwezo kamati za ulinzi wa wanawake na watoto na kuifikia jamii. Pamoja na kwamba mradi wenu umefikia mwisho na kusaidia matukio ya ukatili lakini bado matukio ya ukatili wa kijinsia yapo, tunaomba kama inawezekana mlete mradi mwingine na niwaombe wadau wengine pia wajitokeze kuleta miradi Shinyanga ili kuhakikisha Shinyanga inaondoa ukatili wa kijinsia tuisaidie jamii”,ameongeza.
Amesema serikali itaendelea kushirikiana na Kivulini katika mapambano dhidi ya mimba na ndoa z a utotoni pamoja na ukatili wa kijinsia huku akiwaomba watu wote katika jamii kushirikiano ili kumkomboa mwanamke na mtoto.
“Naomba watu wote waliofikiwa na Kivulini muwe mabalozi wa kuleta mabadiliko. Ukatili hautoki mbali bali upo ndani ya familia, hivyo ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha anapinga mimba na ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto”,amesema.
Hata hivyo ili kuondokana na mila na desturi zinazokwamisha mapambano dhidi ya mimba na ndoa za utotoni na ukatili wa kijinsia ni vyema Viongozi wa Mila pamoja na waganga wa kienyeji washirikishwe ili wawe sehemu ya mabadiliko katika kumkomboa mwanamke na mtoto wa kike.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nice Munissy amesema watatumi pikipiki na baiskeli hizo kwa malengo yaliyokusudiwa huku akiwataka wadau wote katika jamii kulibeba kwa pamoja jukumu la kulinda wanawake na watoto dhidi ya matukio ya ukatili.
Hakimu Mfawidhi wilaya ya Kishapu, Johanitha Projest Rwehabula amesema kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kwenye kesi za matukio ya ukatili wa kijinsia imekuwa ni kikwazo kikubwa hivyo kuchangia kuendelea kuwepo kwa matukio ya ukatili wa kijinsia.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary akizungumza leo Alhamisi Novemba 4,2021 wakati Shirika la Kivulini likikabidhi Pikipiki nne na Baiskeli 50 kwa ajili ya Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa kata za 9 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga zisaidie katika kutoa elimu na ufuatiliaji mashauri ya mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini, Yassin Ally akizungumza leo Alhamisi Novemba 4,2021 wakati akikabidhi Pikipiki nne na Baiskeli 50 zilizotolewa na Kivulini kwa ufadhili wa shirika la OXFAM Tanzania kwa ajili ya Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa kata za 9 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga zisaidie katika kutoa elimu na ufuatiliaji mashauri ya mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Muonekano wa Pikipiki nne na Baiskeli 50 zilizotolewa na Kivulini kwa ufadhili wa shirika la OXFAM Tanzania kwa ajili ya Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa kata za 9 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga zisaidie katika kutoa elimu na ufuatiliaji mashauri ya mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Muonekano wa Baiskeli 50 zilizotolewa na Kivulini kwa ufadhili wa shirika la OXFAM Tanzania kwa ajili ya Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa kata za 9 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga zisaidie katika kutoa elimu na ufuatiliaji mashauri ya mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Muonekano wa Pikipiki nne na Baiskeli 50 zilizotolewa na Kivulini kwa ufadhili wa shirika la OXFAM Tanzania kwa ajili ya Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa kata za 9 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga zisaidie katika kutoa elimu na ufuatiliaji mashauri ya mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Muonekano wa sehemu ya Pikipiki nne na Baiskeli 50 zilizotolewa na Kivulini kwa ufadhili wa shirika la OXFAM Tanzania kwa ajili ya Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsi na Watoto, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Watendaji wa kata za 9 za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga zisaidie katika kutoa elimu na ufuatiliaji mashauri ya mimba na ndoa za utotoni na ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary (katikati) akikata utepe wakati Shirika la Kivulini likikabidhi Pikipiki nne na Baiskeli 50 kwa ajili ya kusaidia kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto halmashauri ya Kishapu na Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nice Munissy akifuatiwa na Mkurugenzi wa shirika la Kivulini, Yassin Ally. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala akifuatiwa na Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Shinyanga, Shillah Moses.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary (katikati) akipiga makofi baada ya kukata utepe wakati Shirika la Kivulini likikabidhi Pikipiki nne na Baiskeli 50 kwa ajili ya kusaidia kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto halmashauri ya Kishapu na Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nice Munissy akifuatiwa na Mkurugenzi wa shirika la Kivulini, Yassin Ally. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala akifuatiwa na Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Shinyanga, Shillah Moses.
Kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la Kivulini, Yassin Ally akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary ufunguo wa pikipiki
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zuwena Omary (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nice Munissy ufunguo wa pikipiki.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nice Munissy (wa pili kushoto) na maafisa wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Dawati la Jinsia na Watoto halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Shinyanga na wakipanda pikipiki baada ya kukabidhiwa na shirika la Kivulini
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nice Munissy akiwa amepakizwa kwenye pikipiki baada ya kukabidhiwa na shirika la Kivulini
Maafisa Watendaji wa vijiji na kata na Wana Mabadiliko wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Nice Munissy akizungumza wakati Shirika la Kivulini likikabidhi baiskeli na pikipiki kwa ajili ya kutokomeza ukatili wa kijinsia.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 Comments