Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMPUNI YA MAURITIUS YAONYESHA NIA KUZALISHA NISHATI YA HDROGEN TANZANIA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Hyrodrogen Partnership Bw. Siegfried Huegemann, Kampuni hiyo imeonyesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa nishati mbadala kwa kutumia gesi ya Hydrogeni. Kushoto ni Dkt. Fred Manyika Afisa Mazingira Mkuu na Dkt. Andrew Komba Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais.

****************************

Na Lulu Mussa, Scotland

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo hii leo amefanya mazungumzo kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya The African Hyrodrogen Partnership Bw. Siegfried Huegemann Glasgow Scotland. Katika maongezi yao Kampuni hiyo imeonyesha nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa nishati mbadala kwa kutumia gesi ya Hydrogeni. Bw. Siegfried Huegemann amesema kampuni yake imedhamiria kuanzisha matumizi ya teknolojia hiyo rafiki kwa mazingira ili iweze kutumika katika sekta ya nishati na usafirishaji.

Ametoa rai kwa Tanzania kuwa tayari kuunga mkono jitihada za kampuni yake katika kuanzisha matumizi ya nishati hiyo barani Afrika na kuwa miongoni mwa nchi chache zinazotarajiwa kunufaika na teknolojia hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo amewakaribisha wawekezaji hao kuwekeza Tanzania na kuwataka kuwasilisha nia yao kwa Sekta zote zinazohusika na masuala ya nishati na uwekezaji.

Mkurugenzi wa Kampuni ya The African Hyrodrogen Partnership yenye makazi yake Port Louis Mauritus ameahidi kuwasilisha rasmi andiko la uwekezaji huo nchini mwishoni mwa mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments