*************************
Ukaguzi wa dawa na Vitendanishi (Commodities Audit) ni jukumu la Msingi la Kila Kamati za usimamizi wa huduma za Afya Mkoa sambamba na zile Kamati za Afya Wilaya (CHMT).
Imekua tabia ya baadhi ya Kamati hizo za Afya kutokufanya ukaguzi huo na kupelekea upotevu/wizi wa dawa na kupoteza mapato ya Serikali ambayo yangetokana na matumizi sahihi ya dawa hizo.
Kufuatia hali hiyo Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe amesema CHMT ambazo hazitafanya ukaguzi wa dawa na vitendanishi (commodities audit), Mganga Mkuu wa halmashauri husika atachukuliwa hatua kwa kukaidi maelekezo ya Serikali.
Amesema Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri wana jukumu la kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa dawa (Medicine Audit) kila robo mwaka kwa mujibu wa sheria na taratibu.
‘Ukaguzi huu wa bidhaa za Afya unatakiwa kushirikisha wakuu wa idara za ukaguzi wa ndani, fedha, manunuzi, mipango na makatibu Tawala wasaidizi,swala hili lisiachiwe idara ya Afya peke yake’ amesisitiza
‘Hakutakuwa na sababu yeyote kwa vituo vyake vya kutolea huduma za afya ambavyo havitafanya ukaguzi wa dawa na taarifa ya kila Mkoa kuwasilishwa Ofisi ya Rais - TAMISEMI.
“ Kwa kufanya ukaguzi wa dawa tutaweza kujua namna dawa zilivyotumika, dawa gani eneo fulani inatumika sana na kwanini na hivyo kubaini mahitaji zaidi kwa wakati unaokuja. Alisisitiza Dkt. Grace
Dkt. Grace aliyasema hayo wakati wa Kikao chake na Kamati ya Usimamizi wa huduma za Afya Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Singida mapema tarehe 14.11.2021 kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
0 Comments