Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalahwa akizungumza na waandishi habari kuhusiana hali ya maji katika mto Ruvu
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Roiner Ilomo akizungumza na wafigaji,Wakulima na watendaji na Madiwano wanaozunguka chanzo cha Maji
Afisa Maji Msaidizi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Dar es Salaam Halima Faraji akizungumza na Wafugaji ,Wakulima ,Madiwani juu hali ya maji ilivyosasa dhidi ya shughuli za kibidamu.
******************************
*Aahidi kutoa ushirikiano kwa kipindi cha uhaba wa maji
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Butamo Ndalahwa,amewapongeza Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu kwa kutoa elimu kwa watendaji wa vijiji, madiwani, wafugaji pamoja na wakulima wa pembezoni mwa Mto Ruvu,jinsi ya utunzaji na uhifadhi wa chanzo hicho cha maji, ili kupunguza makali ya magao wa maji kwa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.
Ndalahwa ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo uliofanyika katika ofisi za halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ambapo mesema kuwa bonde la Wami /Ruvu lina kazi kubwa ya kutoa elimu kwa jamii kuhakikisha chanzo cha Mto Ruvu kinalindwa na kusimamiwa na wadau wote.
Amesema kuwa changamoto kubwa ambayo inashuhudiwa kwa hivi sasa ni kina cha maji katika Mto Ruvu kimepungua na kufanya uhaba wa maji ambapo kumeongeza na shughuli za kibinadamu.
Amesema katika kikao hicho wameweka mkakati wa muda mfupi wa katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji uliopo kwa hivi sasa.
"Moja wapo ya azimio tuliojiwekea ni kuhakikisha tunafikisha elimu, kata, vijiji na vitongoji, tuhakikishe watu wanaelewa umihimu wa Mto Ruvu, watu waweze kuulinda na kutuunzia, lakini pia wafugaji, tumeweza kuongea na wao kuweza kutumia marambo yaliopo katika Kata na vitongoji vyetu ili kupunguza uharibufu kwa kuwa na mifugo mingi," amesema Kwa upande wa Afisa Maji Msaidizi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu Dar es Salaam Halima Faraji amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa kipindi chote kinachofanyika ni kukimbushana tu
Amesema kuwa kwa kipindi hiki wanaangalia namna ya kuhakikisha maji ya yanafika kwa kuwataka wanachi kuacha uvunaji wa maji.mengi kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
0 Comments