Ticker

6/recent/ticker-posts

BONDE LA WAMI/RUVU YAFANYA UKAGUZI WA VYAZO VYA MAJI


Afisa Maji Msaidizi wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Dar es Salaam Halima Faraji akizungumza kuhusiana na maji kupugua katika mto Ruvu wakati bonde hilo lilipofanya ziara Kibaha.

Afisa Mazingira wa Wilaya ya Kibaha Maxmillian Evarist akizungumza kuhusiana na uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji wakati Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu ilipofanya ziara

Shughuli za kibidamu zinazofanywa ndani ya Mto Ruvu.

Ng'ombe wakiwa katika sehemu ya chanzo cha Maji Mto Ruvu katika Kidakio cha Ruvu Chini. Sehemu ya Bwawa la Kidete,Kibaha linaloangaliwa kitaalam wa kutoa maji kuingiza katika Mto Ruvu kukabili ukame ni mara baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara.

*****************************

* Labaini uwepo wa shughuli za Kilimo na Ufugaji katika Mto Ruvu

*Yatekeleza agizo la Waziri Mkuu ya uangaliaji wa uchepushaji wa maji katika Mto Ruvu.

BODI ya Bonde la Wami/Ruvu imefanya ukaguzi katika wakuangali upotevu wa maji katika Mto Ruvu ili kuhakikisha maji yote yanafika kwenye vidakio ili kupunguza makali ya uhaba wa maji kwa Mikoa wa Pwani na Dar es Salaam.

Katika ukaguzi huo, bonde kwa kuaangalia mwingiliano wa shuguli za kibinadamu zinazofanywa katika Mto Ruvu katika Maeneo ya Mlandizi wilayani Kibaha na kusitisha shughuli za wafugaji na wakulima katika kipindi hiki cha uhaba wa maji.

Ukaguzi huo ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilotoa siku tatu kwa bonde hjilo kuhakikisha wanafatilia mwenendo wa maji kutiririka katika mto Ruvu ambazo na kuangalia kama baadhi ya watu wamechepusha maji hayo.

Akizungumza katika ukaguzi Afisa Maji Msaidizi wa Bodi ya Bonde Dar es Salaam, Halima Faraji, amesema kuwa kutokana mabadiliko ya tabianchi yamesababisha maji kapungua katika Mto Ruvu pia huku ikichangiwa na shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika Mto huo.

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu imesema inaangalia uwezekano wa kutoa maji katika Bwawa la Kidete lakini kabla ya kutoa maji hayo lazima yachunguzwe kwenye maabara kuona yanafaa kwa matumizi ya Binadamu.

Amesema bonde limekuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika kuhakikisha maji yanawafikia watumiaji.

"Kilichojitokeza sasa hivi mvua zimekuwa chache kwa mwaka huu, kumekuwa na upiungufu mkubwa wa maji ambao umeathiri Mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro pamoja na Pwani, Kwa kiwango kidogo cha maji ambacho kipo kwenye Mto Ruvu tumehakikisha wananchi wanatumia maji kwa ufanisi kwa kupunguza matumizi," amesema Faraji

Aliongeza kuwa wapo katika mpango wa kushirikiana na Wizara ya Mifugo kuhakikisha wafugaji wanajengewa mabirika na mabwawa ya kunyweshea mifugo kwani maji katika kipindi cha kiangazi yanakuwa madogo ili wasiingie katika mito kunywesha mifugo yao.

Aliongeza kuwa bodi itahakikisha kwa kiwango hicho cha maji kidogo kilichopo kitatumika kwa maji ya kunywa kwa wanachi mpaka pale maji yatakapoongezeka na kufanya huduma zingine kurudi katika hali ya kawaida.

Faraji amesema kwa hali ilipofikia kwa wale ambao hawataki kutii mamlaka watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni kulinda wananchi kuwa na uhakika wa kupata maji ya kunywa.

Aidha amesema kuwa kwa wenye vibali vya kuchota maji katika mto Ruvu kuhakikisha wanapunguza viwango vyao ili maji yaende katika vidakio na kuwafikia watumiaji.

Kwa upande wa Afisa Mazingira wa Wilaya ya Kibaha Maxmillian Evarist amesema katika kipindi hiki cha uhaba wa maji wanaondesha shughuli kando kando ya mto Ruvu waache tu kwani kuendelea na shughuli hizo haileti afya kwa watumiaji ya maji.

Amesema wakulima wanatakiwa kubadili aina ya kilimo kwa kuacha kuvuna maji badala yake watumie kilimo cha umwagiliaji wa matone ambao hautumii maji mengi kutokana na mabadiliko ya Tabaianchi.

"Jambo hili tunafanya kwa masilahi ya taifa kwa ujumla wananchi kuacha kuchepusha maji kinachotakiwa ni kuelimishana na kujengea uwezo katika kuokoa hali ya upungufu wa maji"amesema Evarist.

Amesema kuwa mabwawa yaliyotokana na Mto Ruvu bado ni sehemu ya mto hivyo kuendesha shughuli za kibinadamu kwa kudai mabwawa hayo sio sehemu ya mto ni makosa kwani mabwawa hayo yanaweza kutumika katika kuongeza maji kwenye mto huo.

Evarist amesema hali ya Ruvu Chini ni mbaya ukilinganisha na hali ya Ruvu juu hivyo kunahitajika nguvu zaidi na kupeana elimu ya kuweza kunusuru upatikanaji wa maji kwa wananchi wanatumia kidakio cha Ruvu chini.

Post a Comment

0 Comments