Ticker

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA VIJIJI 400 KUNUFAIKA NA MRADI WA AWAMU YA TATU MZUNGUKO WA PILI MKOANI MTWARA



Afisa Masoko Makao Mkuu TANESCO Bw.Innocent Lupenza,akitoa elimu pamoja kuwahamasisha wananchi wa Mtwara Mjini pamoja na Masasi kuhusu kuchangamkia fursa ya uwekaji umeme katika Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili.


Afisa uhusiano huduma kwa wateja Mkoa wa Mtwara Bw.Jumanne Nkunguu akitoa elimu kwa wananchi wa Mtwara Mjini pamoja na Masasi kuhusu matumizi ya kifaa cha UMETA – umeme tayari kama mbadala wa kufanya wiring katika nyumba ndogo kinachopatikana kwa gharama ya sh 36,000.

.............................................................

Na.Alex Sonna,Mtwara

Jumla ya Vijijini 401 kunufaika na Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili huku zaidi ya vijijini 100 tayari vimepatiwa elimu pamoja na wananchi kutakiwa kuchangamkia fursa ya uwekaji umeme katika Mradi huo.

Pia Zoezi hilo la uhamasishaji wa wananchi pamoja na kupatiwa elimu limefanyika katika maeneo ya Mtwara Mjini,Masasi huku likitarajia kuendelea Nanyumbu.

TANESCO kitengo cha Masoko Makao Makuu kwa kushirikiana na ofisa huduma kwa wateja Mkoa wa Mtwara wameendelea na zoezi la uhamasishaji wa wananchi pamoja na kutoa elimu ili waanze kujianda na fursa hiyo.

Wakitoa Elimu kwa wananchi wamesema kuwa wanufaika wa mradi huo ni wananchi wote watakaofikiwa na miundombinu ya umeme.

”Tunawaomba wananchi wote muwe na subiri kwani huduma ya umeme mtakapata bila shida yoyote na zoezi hilo linatarajia kuwafikia zaidi ya wakazi wa vijiji 100 kati ya 400 vitakavyonufaika na mradi''wamesema

Pia wananchi wametakiwa kutumia wakandarasi au kifaa cha UMETA huku pia hilo limehusisha ofisi za wilaya kwa kupita kwa wakuu wa wilaya pamoja na kushirikiana na maafisa tarafa na wenyeviti na watendaji wa vijiji ili kukomesha utapeli

Lazima mtumie wakandarasi wanaotambulika ili kuepuka matapeli na Ofisi ya Mkoa TANESCO itahakikisha inapeleka orodha hiyo kwenye ofisi ya kila kijiji ili wananchi waweze kupata mafundi sahihi.

Hata hivyo wananchi wametakiwa Kujihadhari na Matapeli/Vishoka kwa kutotoa kiasi chochote cha pesa kwa mtu yeyote ili kuletewa nguzo au kulipia fomu ya maombi ya umeme malipo yote yanafanyika kupitia mfumo rasmi wa malipo ya serikali.

Wananchi wameelezewa kuwa wameanza kwa kushirikiana na ofisi za wilaya kwanza ili kuutambulisha mradi huu wa REA III mzunguko wa II pamoja na kuwatambua wawekezaji wa maeneo hayo ili waweze kutambulishwa TANESCO.

Post a Comment

0 Comments