Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDALICHAKO AZINDUA USAMBAZAJI WA VITABU MIL.20, AWATAKA WALIMU WAWAPE WANAFUNZI


**********************************

Waziri wa elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako leo amezindua kazi ya usambazaji wa vitabu vya kiada vya shule za msingi na Sekondari ambapo amewataka walimu wa Shule zote nchini kuwapatia wanafunzi vitabu hivyo ili waweze kujisomea na endapo mzazi atataka kumnunulia mtoto wake vitabu hivyo vinapatikana.

Wito umeutoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua akizindua kazi ya kusambaza vitabu hivyo, ambavyo vitasambazwa katika Halmashauri zote, amesema walimu hususani wa vijijini wasivifungie ndani vitabu hivyo kwa kuhofia kuchafuka kwani hilo sio lengo la Serikali katika utoaji wa elimu.

"Niwasisitize walimu na wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivi, na endapo ikitoea kuna kitu cha kuongeza katika vitabu hii, basi TET wapo tayari kupokea maoni, ila rai yangu kwenu walimu wapeni vitabu wanafunzi watumie musivifungie ndani."amesema Prof Ndalichako.

Amesema kuwa, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu imetoa shi bill 46 kwa ajili ya uandishi na uchapishaji wa nakala za vitabu zaidi ya mill 20,ambapo vitabu hivyo vitasaidia kutoa muongozo kwa walimu jinsi ya ufundishaji na kuwapatia fursa wanafunzi kuweza kujipima kwa maswali.

Aidha, amesema kuwa awali kuliwa na changamoto ya upungufu wa vitabu lakini kupitia nakala hizo tatizo hilo linakwenda kumalizika, ambapo kuna baadhi ya shule vitabu vimeharibika hivyo vitakwenda kufidia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elim Tanzania (TET) Aneth Komba amesema katika vitabu vitakavyo sambazwa, kwa ngazi ya Secondary Serikali kupitia mapato yake ya ndani imetoa shill bill 15.8 kwa ajili ya uchapishaji na uandishi ambapo kazi hiyo imefanywa wataalamu wabobez wa ndani kwa kushirikiana na Sekta binafsi.

Aidha, ameishukuru Serikali wa wamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujenga uhusiano mzuri na wadau wa maendeleo kwa kuchangia Sekta ya elimu.

Ameongeza kuwa, Ili kuhakikisha Taasisi hiyo inapata mrejesho wa haraka wa usambazaji wa nakala hizo wameandaa mfumo rasmi kwa ajili kupokea taarifa ambapo Afisa elimu ngazi ya Halmashauri atajaza takwimu za nakala alizopokea.

Naye, Naibu Katibu Mkuu elimu (NKE) Gerald Mweri amesema hii ni mara ya kwanza kusambaza vitabu vingi namna hiyo, ambapo ameahidi nakala mill 20 zitasambazwa ndani ya wiki moja na kuhakikisha zinafika Halmashauri zote nchini.

"Nikuahidi Waziri wa Elimu, tumejipanga vizuri mara niliposkia kuna vitabu vinakuja niliungana na timu yangu ya maafisa elimu,vitabu hivi vitakapofika shuleni vitatumika na tumeshajipanga kuvisambaza nchi nzima.

Amesema kuwa, kuwepo kwa vitabu hivyo,vitawasaidia walimu kuwapa muongozo pamoja na kwenda kuimarisha ufundishaji ambapo watatumia rasimali hizo ili watoto wasome kwani hiyo ndio faida ya Serikali.

Aidha, ametoa agizo walimu wawape vitabu wanafunzi vitabu kwa kuwaandikisha ili waende navyo nyumbani kwa ajili ya kujisomea na hatimae waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

Post a Comment

0 Comments