Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIR WA AFYA DKT GWAJIMA AMEKUTANA NA WATOA HUDUMA WA AFYA KITENGO CHA MACHO


*******************************



Na Richard Mrusha




Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt,Dorothy Gwajima leo tarehe 04,10, 2021 amekutana na watoa huduma za magonjwa ya Macho kwa lengo la kujadili mikakati ya kuboresha huduma za macho hapa nchini kuelekea maadhimisho ya siku ya Afya ya Macho Duniani.




Dkt Gwajima amekutana na Wadau hao leo Jijini Dar es salaam, na amesema kuwa Maadhimisho hayo mwaka huu 2021 yenye kauli mbiu isemayo "Yapende Macho yako" Nenda kapime sasa Kwa kuwa kila mtu anahisika kulinda Afya yake ambapo kitaifa yatafanyika Jijini Dodoma Oktoba mwaka uhu.




Dkt Gwajima amesema kuwa ameanza kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan aliyeagiza kuwepo kwa ushirikiano kati ya Serikali na Wadau kufanya kazi kwa pamoja ili Kuwafikia watu wenye uhitaji kwenye maeneo yao

Post a Comment

0 Comments