Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela akizungumza katika maadhimisho ya miaka 11 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo. Hafla hiyo imefanyika jana katika hospitali ya Heamed iliyopo Bunju B Jjijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Heameda Bi.Edwina Lupembe akizungumza katika maadhimisho ya miaka 11 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo. Hafla hiyo imefanyika jana katika hospitali ya Heamed iliyopo Bunju B Jjijini Dar es Salaam.
Muuguzi wa Hospitali ya Lugalo Luteni Kanali Pius Horumpende akizungumza katika maadhimisho ya miaka 11 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo. Hafla hiyo imefanyika jana katika hospitali ya Heamed iliyopo Bunju B Jjijini Dar es Salaam.
Afisa Mahusiano wa Benki ya CRDB Bw.Horuma Naftal akizungumza katika maadhimisho ya miaka 11 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo. Hafla hiyo imefanyika jana katika hospitali ya Heamed iliyopo Bunju B Jjijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi Bw.Respige Kimati akizungumza katika maadhimisho ya miaka 11 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo. Hafla hiyo imefanyika jana katika hospitali ya Heamed iliyopo Bunju B Jjijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela akipata picha ya pamoja na watumishi wa hospitali hiyo katika maadhimisho ya miaka 11 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo. Hafla hiyo imefanyika jana katika hospitali ya Heamed iliyopo Bunju B Jjijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wananchi wanapaswa kupewa elimu juu ya umuhimu wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kujikinga na maradhi kabla hayajawa sugu.
Ameyasema hayo jana Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Heameda Dkt.Hery Mwandolela katika maadhimisho ya Miaka 11 toka kuanzishwa kwa hospitali hiyo iliyopo Bunju B Jijini Dar es Salaam.
Amesema ni muhimu kuwa na mifumo mizuri ya maisha ikiwemo kula chakula kinachotakiwa na kufanya mazoezi ili kuepukana na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.
"Tumekuwa tukitoa Elimu ya Afya huusan ya magonjwa ya moyo kupitia vipindi vya afya ITV, Radio One, TBC, Clouds Tv na Redio, Upendo Tv na kwa kupitia magazeti mbalimbali kama mwananchi". Amesema
Aidha amesema hospitali hiyo ina changamoto nyingi ikiwemo ubovu wa barabara inayoingia hospitalini kuwa kero kwa wagonjwa na wafanyakazi haswa kipindi cha mvua, taarifa hizi wamezifikisha katika mamlaka husika kwa hatua zaidi.
Amesema matarajio yao kumaliza ujjenzi kwa sehemu iliyobaki, kufungua Chuo cha mafunzo ya kada mbalimbali za afya kwa kiwango cha stashahada (Diploma) na hapo baadae kuwa Chuo Kikuu cha Afya.
"Hospitali ya Heameda imefanikiwa kufikia malengo iliojiwekea ikiwemo kutoa huduma bora za kisasa kwa asilimia 90%". Amesema
Pamoja na hayo amesema hospitali imeweza kutoa huduma ya elimu ya afya na upimaji kwa taasisi binafsi na za Serikali ikiwemo Benki ya Tanzania, TANESCO, CRDB, TTCL, TANTRADE, NMB, COCACOLA na Vodacom ambao wote ni wateja wao katika kuwapa huduma wafanyakazi wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi Bw.Respige Kimati amesema watakuwa wakishirikiana na hospitali ya Heameda kuhakikisha huduma zinatolewa vizuri kulingana na mahitaji.
"Tutashirikiana na hospitali hii mpaka pale tutakaposema basi kwa maana kufikia malengo makubwa. Tunataka hospitali hii iwe na hadhi kubwa kama hospitali zingine kwani mpaka sasa huduma zinazotolewa na nzuri na ni kubwa kama hospitali zingine ambazo ni kubwa". Amesema Bw.Kimati.
Nae Muuguzi wa Hospitali ya Lugalo Luteni Kanali Pius Horumpende ameushukuru uongozi wa hospitali ya Heamed kuhakikisha huduma ambazo wanazitoa ni bora ukilinganisha na hospitali kubwa ambazo zinatoa huduma kama zinazotolewa na hospitali hiyo.
0 Comments