Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc anayemaliza muda wake Hisham Hendi (kulia) akimtambulisha mkurugenzi mkuu mpya ajaye Sitholizwe Mdlalose (Kushoto) kwa wanahabari waliohudhuria mkutano wa kuwaaga ulioandaliwa bwana Hisham. Kwenye mkutano huo, Hisham aliwashukuru wanahabari kwa ushirikiano waliompa katika kipindi cha uongozi wake, huku akiwaomba kumuunga mkono Sitholizwe katika juhudi zake za kuboresha huduma kwa wateja nchini na hivyo kuiletea maendeleo Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc Sitholizwe Mdlalose akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kutambulisha kwake jijini Dar es Salaam hap oleo. Mdlalose aliwaomba waandishi wa Habari wampe ushirikiano kama waliokuwa wanampa mtangulizi wake Hisham Hendi.
0 Comments