Ticker

6/recent/ticker-posts

UJENZI YAICHARAZA RAS RUVUMA GOLI 33 KWA 21 


Wachezaji wa timu ya mpira wa pete kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, ( Sekta ya Ujenzi), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuingia uwanjani na kukabiliana na wapinzani wao RAS Ruvuma, katika Mashindano ya SHIMIWI, yanayofanyika mkoani Morogoro .


Wafungaji mahiri wa magoli kutoka timu ya mpira wa pete Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Bi Kaundime Kizaba anayechezea nafasi ya (G.S) akisaidia na Bi Jesca Mndaba anayecheza nafasi ya ( G.A), wakiwania mpira dhidi Wapinzani wao RAS Ruvuma wakati wa mechi za Makundi.


Wachezaji wa Timu ya mpira wa pete kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,( Sekta ya Ujenzi), waliovaa sare ya damu ya mzee, wakikabiliana vikali dhidi ya wapinzani wao RAS Ruvuma na kuibuka na ushindi wa magoli 33 kwa 21, katika michezo ya SHIMIWI, Mkoani Morogoro.

Baadhi ya Mashabiki wa timu ya sekta ya Ujenzi, wakiimba na kucheza mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 33 kwa 21 dhidi ya RAS Ruvuma, Mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.

**********************************

Timu ya mpira wa pete kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,(Sekta ya Ujenzi), yaibuka kidedea kwa goli 33 kwa 21 dhidi ya wapinzani wao Ofisi ya Katibu tawala Mkoa wa Ruvuma ( RAS-RUVUMA).



Akizungumza katika mashindano ya Michezo ya Idara na wizara za Serikali (SHIMIWI), yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, kocha wa Timu ya Ujenzi Bi Mwamvita Mzee, amesema kuwa katika kipindi cha kwanza Ujenzi iliongoza kwa magoli 14 huku RAS -RUVUMA ikiwa nyuma kwa mabao 12 na magoli yaliyosalia yalifungwa kipindi cha pili cha mchezo huo.



Aidha, kocha huyo ameongeza kuwa wamejipanga vizuri na wanatarajia kupata ushindi zaidi katika michuano mingine ya makundi huku wakiwa na kauli mbiu 'anayekuja na achapwe'.



Katika mchezo mwingine, Timu ya Mpira wa pete ya Sekta ya Ujenzi sikuya Jumamosi tarehe 23 mwezi huu inatarajia kucheza na Wizara ya Mambo ya nje katika viwanja vya Jamhuri Mkoani Morogoro.

Post a Comment

0 Comments