Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Christian Blind Mission Tanzania (CBM) Bi Nesia Mahenge,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Oktoba 23,2021 wakati akitoa taarifa kuelekea Wiki ya Maonyesho ya AZAKI 2021 yanayotarajia kuanza kesho Oktoba 23 hadi 28,2021 jijini Dodoma. Mkurugenzi Mtendaji United Nations Association of Tanzania Reynald Maeda,akielezea Wiki ya Maonyesho ya AZAKI 2021 yanayotarajia kuanza kesho Oktoba 23 hadi 28,2021 jijini Dodoma.
......................................................................
Na Juhudi Mmari,Dodoma
SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai kesho anatarajia kufungua wiki ya Asasi za Kiraia(AZAKI)ambapo jumla ya Asasi zaidi ya 150 zitashiriki katika maonyesho lengo likiwa ni kuonyesha mchango wake katika maendeleo ya Taifa.
Akizungumza jijini Dodoma Mkurugenzi mkazi wa Christian Blind Mission (CBM) Nesia Mahenge wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu kuelekea wiki ya AZAKI amesema wiki hiyo inakusudia kuonyesha namna asasi za kiraia zilivyo natija katika kuleta maendeleo ya Taifa Bi.Mahenge amesema, wiki ya Azaki imekusudia kuwaleta wadau mbalimbali wa Maendeleo nchini ikiwemo Wananchi,Serikali, na sekta binafsi ambapo itasaidia kwa pamoja kujadili na mstakabali na mchango wa AZAKI katika kuleta maendeleo nchini.
"Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kujumuika nasi kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali pamoja na kuwajengea uwezo wakujua namna Azaki inavyotekeleza majukumu yake kwenye Nyanja ya maendeleo,"amesema.
Pamoja na hayo Mahenge ameeleza kuwa uzinduzi huo wa wiki ya AZAKI utahudhiriwa na wahisani wa maendeleo wakiwemo ubalozi wa Denmark Utakaowakilishwa na Sascha Mulla na Ubalozi wa Canada utawakikishwa na Ms.Helen Fytche.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa United Nations Association (UNA) Reynald Maeda ameweka bayana Viongozi na wageni mbalimbali kutoka Serikalini watakaoshiriki katika uzinduzi huo ni pmaoja na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri,Meya wa Jiji la Dodoma Prof.Davis Mwamfupe na mwakili kutoka Wizara ya Afya Vickness Mayao.
Kwa mujibu wa mkurugenzi maendeleo yanayoletwa na AZAKI si maendeleo ya kifedha tu bali katika maeneo mengine ikiwemo maendeleo ya wanachi kupitia miradi mbalimbali ikiwemo kuongeza ushirikishwaji wa watu wote kwenye jamii,kupinga ukatili wa kijinsia Kwa wanawake na Watoto pamoja na kuongeza nguvu katika ufuatikiaji wa rasilimali za umma.
0 Comments