Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA YANG'ARA UGENINI LIGI YA MABINGWA YAICHAPA 2-0 JWANENG GALAXY YA BOTSWANA


.................................................................... 

Wawakilishi wa Tanzania katika Michuano ya Klabu bingwa Afrika timu ya Simba imewaduwaza wenyeji Jwaneng Galaxy baada ya kuwachapa mabao 2-0 mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya kwanza uliochezwa katika uwanja wa Taifa Gaborone nchini Botswana. 

Shujaa wa Simba alikuwa mshambuliaji hatari John Bocco baada ya kufunga mabao yote mawili dakika ya 2 na 5. 

Kwa ushindi huo Simba wamejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi huku Jwaneng wakiwa na kibarua kizito cha kupindua meza katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Octoba 24, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 

Huku Simba wakihitaji sare au ushindi wa aina yeyote ili kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Post a Comment

0 Comments