Ticker

6/recent/ticker-posts

SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE YA 0-0 NA COASTAL UNION



***************************

Na.Emmanuel Mbatilo,Dar es Salaam

Mabingwa watetezi wa Tanzania timu ya Simba imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kubanwa mbavu ya bila kufungana na wagosi wa kaya Coastal Union kutoka Tanga mchezo wa Ligi ya NBC uliopigwa katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Timu zote zilianza kwa kucheza mpira wa kushambuliana huku Coastal wakicheza rafu zilizopelekea wachezaji wa Simba Kuumia.

Mara baada ya kuumia kwa wachezaji hao kipindi cha kwanza Simba ililazimika kufanya mabadiliko ya lazima kwa Sadio Kanoute na Muzamiru Yassin huku nafasi zao kuchukuliwa na Jonas Mkude na Benard Morrison.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kushambuliana huku Simba wakiongeza mashambulizi yakiongozwa na John Bocco,Meddie Kagere na Yusuph Mhilu.

Dakika ya 72 Coastal walipata pigo baada ya mchezaji wao Jacoeb Benedicto kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kisha nyekundu licha ya kuwa pungufu Coastal walianza kucheza mchezo wa kushambulia na kujilinda na kukalibisha mashambulizi zaidi langoni kwao.

katika dakika za nyongeza beki wa Simba Henoc Inonga alioneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea faulo mchezaji wa Coastal.

Kwa matokeo hayo Simba wamefikisha pointi 8 kwa kucheza mechi nne na kupanda nafasi ya nne huku Coastal wakifikisha pointi 3 katika nafasi ya pili.

Yanga bado wanaongoza Ligi hiyo wakiwa na Pointi 12 wakiwa wamecheza mechi nne na hawajapoteza hata mechi moja pamoja na kutoruhusu nyavu zao kutikiswa.

Post a Comment

0 Comments