Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA).
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amefungua Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja ili kutoa mwongozo kwa mnufaika/mteja na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) kila upande ujue haki na wajibu wake huku akiwataka wadau kutoa maoni na kuacha kulalamika tu.
Warsha hiyo imefanyika leo Jumatano Oktoba 20,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maji ambao wametoa maoni yao kuhusu Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja.
Mkuu huyo wa wilaya amesema dhana ya kuwa na Mkataba wa Huduma kwa Wateja inatokana na ukweli kwamba utoaji wa huduma kwa wananchi una changamoto nyingi na changamoto zinazokabili utoaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi mara nyingi zinahitaji juhudi za pamoja katika kuzitafutia ufumbuzi.
“Warsha hii ni njia mojawapo ya kuhakikisha kwamba wanufaika kwa huduma zinatolewa na SHUWASA wana uelewa mpana kuhusu haki na wajibu wao. Ni matarajio ya wateja kuwa huduma itakayotolewa itazingatia viwango vya ubora vinavyostahili”,amesema Mboneko.
“Kuandaliwa kwa warsha hii ni ushahidi tosha kuwa SHUWASA inajali wateja wake.Warsha hii itapanda mbegu za matumaini ya kujenga mshikamano na ushirikiano katika masuala yote yanayohusu njia bora zaidi kuendeleza huduma ya maji. Naomba vipengele vyote vijadiliwe kwa umakini wa hali ya juu na maoni yenu yatawasilishwa kwenye ngazi zingine katika mlolongo wa mchakato wa maandalizi ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja”,amesema Mboneko.
Katika hatua nyingine Mboneko ameipongeza SHUWASA kwa huduma bora ya maji inayoendelea kutoa katika wilaya ya Shinyanga na kuiomba kuongeza kasi ya usambazaji huduma ya maji kwenye maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo.
Awali akizungumza katika Warsha hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola amesema SHUWASA ina jumla ya wateja 25,357 kwa wakazi takribani 252,970.
Mbali na kuhudumia Manispaa ya Shinyanga maeneo mengine ya usimamizi ambayo SHUWASA inatoa huduma ni Tinde, Didia na Iselamagazi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na inasimamia mradi wa maji safi wa Ngogwa – Kitwana halmashauri ya Manispaa ya Kahama na inaendelea kutekeleza miradi ya Mwawaza – Negezi na IFF –OBA, Bujinge,Mwalugoye,Ibadakuli, Busongo,Masekelo, Ndembezi na Butengwa.
Pia amesema kila ifikapo Tarehe 20 ya kila mwezi SHUWASA imekuwa ikitoa bili za maji huku akiwaomba wateja kuendelea kutoa maoni mbalimbali ili kuboresha huduma za maji sambamba na kuwaomba kulipa bili kwa wakati ndani ya siku 30 zinazotolewa na SHUWASA wateja kulipa bili.
Aidha amezitaja bei za Unit kuanzia o hadi 5 ni shilingi 1420/= kwa manispaa ya Shinyanga tu, na kuanzia Unit 6 bei ni shilingi 1650/= kwa kila Unit.
Mhandisi Katopola amesema Rasimu ya Mkataba ni mchakato wa Mamlaka ya Uthibiti na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambapo baada ya kikao hicho itarudishwa EWURA kwa ajili ya kupitiwa huku matarajio yakiwa ni kuboresha huduma ya maji safi katika Mji wa Shinyanga na maeneo mengine.
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi amewashukuru wadau kujadili Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja na kutoa mapendezo mbalimbali ili kuboresha huduma za maji kwenye maeneo ambayo SHUWASA inafanya shughuli zake huku akiwaomba wadau kuendelea kushirikiana na SHUWASA na kutosita kutoa ushauri kama kuna changamoto imejitokeza na ikiwa ni pamoja kutoa taarifa wanapoona kuna uvujaji wa maji kwenye mabomba.
Nao wadau walioshiriki warsha hiyo wameishukuru SHUWASA kwa kuendelea kuwa karibu na wateja wao na kuomba kuwa ubunifu zaidi ili kuboresha huduma za maji wilayani Shinyanga.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) leo Jumatano Oktoba 20,2021 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza wakati akifungua Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuph Katopola akizungumza kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na SHUWASA.
Mwenyekiti wa Bodi ya SHUWASA Bi. Mwamvua Jilumbi akizungumza kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na SHUWASA.
Afisa Uhusiano na Umma wa SHUWASA Bi. Nsianel Gelard akiwasilisha Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja
Afisa Rasilimali Watu wa SHUWASA, Kambira Mtebe akizungumza kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Mhe. Boniphace Chambi akiongoza kikao cha kujadili Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja
Mwanasheria wa SHUWASA Happy Richard akizungumza kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja iliyoandaliwa na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Maafisa wa SHUWASA wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Wadau wa Maji wakiwa kwenye Warsha ya Wadau wa Maji kwa ajili ya kupitia Rasimu ya Mkataba wa Huduma kwa Wateja baina ya Wateja na SHUWASA.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
0 Comments