Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MAKALLA: TUTARUHUSU MRADI WA STENDI MWENGE, UWANJA WA MPIRA NA JENGO LA UTAWALA MANISPAA YA KINONDONI KUENDELEA KUJENGWA.


*******************************

- Apongeza hatua zilizochukuliwa na Waziri Ummy Mwalimu.

- Asema kasoro zilizojitokeza zimerekebishwa Na Muda wowote kuanzia Sasa atatoa Barua ya kuelekeza kuendelea kwa Miradi hiyo.

- Awapongeza Manispaa ya Kinondoni kwa kutekeleza Miradi mikubwa kwa Mapato ya ndani.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametembelea Miradi Mitatu ambayo ilielekezwa kusimama Ujenzi na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu Kutokana na kasoro zilizoonekana ambapo amesema muda wowote kuanzia Sasa atatoa Barua ya kuelekeza kuendelea kwa Miradi hiyo.

Miongoni mwa Miradi hiyo ni Jengo la utalawa Manispaa ya Kinondoni linalogharimu Bilioni 2, Uwanja wa Timu ya KMC na Kituo Cha Daladala Cha Mwenge.

Aidha RC Makalla amesema baada ya kuruhusu kuendelea kwa Ujenzi anataka kuona kazi ifanyike kwa ushirikiano, kuaminiana na wataalamu wote kushauri kitaalamu ili lengo la Serikali liweze kutimia.

Hata hivyo RC Makalla ameelekeza Manispaa ya Kinondoni kuepuka kuwa na Miradi mingi ya kutekeleza kiasi kwamba wanashindwa kutawanya fedha Jambo linalosababisha kuchelewa kumalizika kwa Miradi hiyo.

Pamoja na hayo RC Makalla amesema Katika ziara ya Leo amejiridhisha kuwa mapendekezo yaliyotolewa na Kamati yalikuwa sahihi na hatua alizochukuwa Waziri Ummy Mwalimu zikikuwa sahihi na amesema atasimama kidete kuhakikisha Miradi hiyo inakamilika kwa wakati na ubora.

Post a Comment

0 Comments