*********************************
- Asema Tamasha limefanikiwa kwa 100%.
- Atangaza Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa kuzindua rasmi Tamasha hilo.
- Awabatiza Wafanyabiashara wa Coco jina la Watoto wa Rais Mama Samia na kuwahakikishia hakuna atakaeondolewa.
- Wananchi Wafurahia Burudani na kupongeza ubunifu uliotumika.
Mamia ya Wananchi na wapenzi wa Burudani wamefurika kwa wingi kwenye Tamasha kubwa la Burudani la DAR SUNSET CARNIVAL Coco Beach ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Tamasha hilo litazinduliwa rasmi na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
Akizungumza wakati wa Tamasha hilo RC Makalla ametangaza kuwa siku ya uzinduzi rasmi kutakuwa na Surprise nyingi za Burudani hivyo amewataka Wananchi kukaa mkao wa kula.
Aidha RC Makalla amesema tukio la leo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa Kutokana na ubunifu wa Maandalizi na mwamko mkubwa wa Wananchi waliojitokeza.
Hata hivyo RC Makalla amesema Maboresho ya ufukwe wa Coco umewezesha kuwa na uwezo wa kuchukuwa zaidi ya Wafanyabiashara 600 kutoka 200 waliokuwepo ambapo amebainisha kuwa lengo la Serikali ni kukuza utali wa fukwe kupitia fukwe zote za Mkoa huo.
Pamoja na hayo RC Makalla amepongeza Kampuni zote zilizokubali kushirikiana na Serikali kujenga Vibanda vya kisasa bure na kusema matatajio ni kuona wiki ijayo Ujenzi wa Vibanda vyote vinakamilika.
Maboresho ya ufukwe wa Coco Beach imejumuisha Usafi wa fukwe, Ujenzi wa Vibanda vya kisasa, Ujenzi wa vyoo, Miundombinu ya Maji, Umeme na kuhakikisha huduma zote za Kifedha zinapatikana eneo Hilo.
0 Comments