Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA KUZINDUA BARABARA SIHA, MTENDAJI MKUU WA TANROADS AKAGUA MAANDALIZI


Mkuu wa Wilaya ya Siha Ndugu Thompson Mwang'onda akisalimiana na Eng. Rogatus Mativila Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wakati Mtendaji huyo alipowasili Wilayani Siha kwa ajili ya kukagua kipande cha Barabara ya Sanya Juu-Elerai iliopo wilaya ya Siha, Kilimanjaro chenye urefu wa kilometa 32.2 ambayo inatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Oktoba 15, 2021.


Eng. Rogatus Mativila Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akiongozana na Eng. Motta Kyando Meneja wa TANROADS mkoa wa Kilimanjaro wakikagua kipande cha Barabara ya Sanya Juu-Elerai iliopo wilaya ya Siha, Kilimanjaro chenye urefu wa kilometa 32.2 ambayo inatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Oktoba 15, 2021.

Eng. Rogatus Mativila Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akiongozana akipata maelezo kutoka kwa Eng. Motta Kyando Meneja wa TANROADS mkoa wa Kilimanjaro wakati akikagua kipande cha Barabara ya Sanya Juu-Elerai iliopo wilaya ya Siha, Kilimanjaro chenye urefu wa kilometa 32.2 ambayo inatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Oktoba 15, 2021.


Eng. Rogatus Mativila Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akitoa maelekezo kwa Eng. Motta Kyando Meneja wa TANROADS mkoa wa Kilimanjaro wakikagua maandalizi ya jiwe la msingi la ufunguzi wa kipande cha Barabara ya Sanya Juu-Elerai iliopo wilaya ya Siha, Kilimanjaro chenye urefu wa kilometa 32.2 kulia ni Charles Lubazibwa Mkaguzi wa barabara na Mwaya Gibson kutoka TANROADS.


Eng. Rogatus Mativila Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akiongozana na Eng. Motta Kyando Meneja wa TANROADS mkoa wa Kilimanjaro wakimsikiliza Injinia Charles Lubazibwa ambaye ni mkaguzi wa barabara wakati akitoa maelezo kuhusu ukamilishaji wa maandalizi ya jiwe la ufunguzi wa barabara hiyo.


Eng. Rogatus Mativila Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akiwa na Eng. Motta Kyando Meneja wa TANROADS mkoa wa Kilimanjaro wakisalimiana na askari wa usalama barabarani wa wilaya ya Siha.


Eng. Rogatus Mativila Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akikagua jiwe la Ufunguzi wa barabara hiyo.


Eng. Rogatus Mativila Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) akipata maelezo kutoka kwa Eng. Motta Kyando Meneja wa TANROADS mkoa wa Kilimanjaro alipokagua eneo litakalofanyika hafla ya ufunguzi wa barabara hiyo.


Muonekano wa kipande cha Barabara ya Sanya Juu-Elerai iliopo wilaya ya Siha, Kilimanjaro chenye urefu wa kilometa 32.2 ambayo inatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Oktoba 15, 2021.


Katika picha ni wafanyakazi wa TANROADS Mwaya Gibson kulia na Bi Lela Muhaji pamoja na Mhandisi Miraji Lubuva Mhandisi Mradi wakiwa katika maandalizi ya tukio hilo.

............................................

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua kipande cha barabara ya SanyaJuu-Elerai iliopo wilaya ya Siha, Kilimanjaro chenye urefu wa kilometa 32.2

Kipande hicho ni sehemu ya ujenzi na ukarabati wa barabara kubwa yenye urefu wa kilometa 98.2 unaotekelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambacho ni kutoka Bomang’ombe-SanyaJuu-Kamwanga.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Rogatus Mativila amesema ufunguzi wa barabara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi mwaka CCM 2020/25.

Eng; Mativila amesema TANROADS imedhamiria kuhakikisha inasimamia kwa ukamilifu ujenzi wa madaraja na barabara mbalimbali nchini ili kuhakikisha inatimiza ndoto ya Serikali kuwa na miundombinu bora ya barabara na madaraja.

“TANROADS imedhamiria kumaliza barabara zote kwa wakati hasa zile za kimkakati ili kutimiza azma ya serikali katika kuharakisha maendeleo na kufungua mikoa kwa mikoa na nchi zingine’’ amesema Eng. Mativila

Amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha za ujenzi wa barabara nchini lengo kubwa la TANROADS ni kuhakikisha barabara hizo zinakuwa bora na kudumu kwa muda mrefu zaidi.

‘’Barabara zinazojengwa sehemu mbalimbali pamoja na hii inayotarajiwa kuzinduliwa na Mheshimiwa Rais Samia Imesanifiwa kudumu kwa miaka 20 , hivyo wananchi wana wajibu mkubwa wa kuitunza na kuilinda’’ alisema Eng. Mativila.

Kwa upande wake, Mhandisi Mradi wa barabara hiyo, Eng. Miraji Hassan alisema barabara itakafunguliwa na Rais Samia ni kipande cha kilometa 32.2 ambacho kimejengwa kwa gharama ya sh. Bilioni 60

Eng. Hassan alisema mradi mzima wa barabara hiyo ni kilometa 98.2 na uligawanya kwa awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza ilikuwa Bomang’ombe-SanyaJuu ambayo ilikuwa kilometa 24, ambapo sehemu kubwa ya barabara hiyo ilifanyiwa ukarabati.

Aidha, alisema sehemu ya pili ilikuwa na ujenzi wa barabara kutoka SanyaJuu – Elerai yenye kilometa 32.2, ambayo inatarajiwa kufunguliwa na Rais Samia huku sehemu ya tatu ni kutoka Elerai-Kamwanga, ambapo usanifu wa barabara hiyo uko tayari kutoka Tanzania hadi mpakani Kenya.

Post a Comment

0 Comments