Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI NA KUMUAGA RAIS WA BURUNDI MHE.NDAYISHIMIYE KUELEKEA NCHINI KWAKE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb) kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Pauline Philipo Gekul (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Eng. Kundo Endrea Mathew (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Jaji Jacob Casthom Mwatembela Mwambengele kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Ndugu. Asina Abdallah Omar kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb) wa kwanza kulia, Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Philipo Gekul (Mb), Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Eng. Kundo Endrea Mathew (Mb) Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jacob Casthom Mwatembela Mwambengele, Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu. Asina Abdallah Omar wakila kiapo cha Maadili ya Utumishi wa umma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kumuapisha Waziri, Naibu Mawaziri katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakizungumza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati wa Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake hapa Nchini.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 mara baada ya Rais huyo wa Burundi Mhe. Ndayishimiye kuhitimisha zira yake nchini na kurejea Burundi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mke wa Rais Evareste Ndayishimiye wa Burundi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake leo tarehe 24 Oktoba, 2021. kulia ni Rais wa Ndayishimiye wa Burundi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake leo tarehe 24 Oktoba, 2021. PICHA NA IKULU.

Post a Comment

0 Comments