Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AKIONDOKA NCHINI KUELEKEA GLASGOW SCOTLAND KUHUDHURIA MKUTANO WA COP 26


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Chumba cha mapumziko Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 30 Oktoba 2021 alipokua akiondoka nchini kuelekea Glasgow, Scotland kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto Duniani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisindikizwa na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alipokua akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 30 Oktoba 2021 kuelekea Glasgow, Scotland kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na jitihada za kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa ili kupunguza joto Duniani

Post a Comment

0 Comments