Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS MHE.DKT.HUSSEIN ALI MWINYI ASHIKIKI KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU WILAYANI CHATO MKOANI GEITA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi wakiwa katika uwanja wa Magufuli katika hafla ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wilayani Chato Mkoa wa Geita.(Picha na Ikulu)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge, Uratibu Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Joakim Mhagama, akizungumza wakati wa hafla ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi wakifuatilia Vijana wa Halaiki wakionesha maumbo mbalimbali, wakati wa Kilele cha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato leo 14-10-2021.(Picha na Ikulu)

VIJANA wa Halaiki kutoka Mkoa wa Geita wakionesha onesho la Mlima Kilimanjaro ukiwa na Mwenge wa Uhuru ukimurika katika mipaka yote ya Tanzania, wakati wa Kilele cha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru Kitaifa na kumbukizi za Kifo cha Baba wa Taifa Marehemu Mwalimu Julius Nyerere na Wiki ya Vijana.hafla hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Magufuli Wilayani Chato.(Picha na Ikulu)

BAADHI ya Viongozi wa Dini na Wananchi wakifuatilia Kilele cha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika katika Uwanja wa Magufuli Chato Mkoani Geita leo 14-10-2021, mgeni rasmin akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwahutumia katika hafla hiyo ya Kilele ya Mbio za Mwenye wa Uhuru Kitaifa Mkoani Geita.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akifuatilia hafla ya Kilele cha Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru, zilizofanyika katika Uwanja wa Magufuli Chato Mkoani Geita na (kushoto) Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na Mjane wa Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere. Mama Maria Nyerere.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakisalimiana na Mawaziri wa SMT na SMZ , baada ya kuwasili katika Uwanja wa Magufuli Chato kuhudhuria hafla ya Kilele cha Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru na Kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Maadhimisho ya Wiki ya Vijana.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments