Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS ALHAJ DKT.HUSSEIN MWINYI AJUMUIKA NA WANANCHI WA MKWAJUNI KIDOMBO KATIKA DUA MAALUM NA KISOMO CHA HITMA


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akitia ubani kuashiria kuanza kwa dua Maalum ya kisomo cha hitma kuwaombea waliotangulia mbele ya haki, dua iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Mkwajuni Kidombo, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa, (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla (kushoto kwa Rais) Mtoto wa Rais wa Zanzibar Mstaafu wa Awamu ya Tano Alhaj. Dk.Salmin Amuor Juma.Ndg.Amini Salimin Amour.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Mkwajuni Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja katika kisomo na dua Maalum kuwaombea Waliotangulia mbele ya haki, iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo, dua hiyo inayokwenda sambamba na Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) na (kulia kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman na (kushoto kwa Rais) Ndg. Amini Salimin Amour, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj.Othman Masoud Othman, Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj. Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.(Picha na Ikulu)

WANANCHI wa Mkwajuni Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja wakijumuika katika dua Maalum na kisomo cha Hitma iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo, inayokwenda sambamba na Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) hufanyika kila mwaka.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akimsalimia Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Alhaj Dk.Salmin Amour Juma, alipofika nyumbani kwake Kijijini Kwao Kidombo Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakati wa hafla ya Kisomo cha Dua Maalum iliofanyika katika Msikiti wa Ijumaa Kidombo na (kushoto ) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Husseinn Ali Mwinyi, baada ya dua hiyo inayokwenda na sambamba na Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad.(S.A.W) hufanyika kilia mwaka katika Kijiji cha Kidombo Mkwajuni Unguja.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume.(hayupo pichani) na (kushoto kwa Rais) Rais Mstaafu wa Zanzibar Awamu ya Tano Alhaj Dk.Salimini Amour Juma, Rais Mstaafu wa Tanzania Awamu ya Pili Alhaj.Ali Hassan Mwinyi na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.Alhaj Othman Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla, wakiitikia dua hiyo, baada ya kumaliza kumsalimiana kumjulia hali nyumbani kwake Kijiji cha Kidombo Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments