Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS ALHAJ DKT. MWINYI AJUMUIKA NA WAUMINI WA KIISLAM KATIKA MAULIDI YA KUZALIWA MTUME MUHAMMAD S.A.W

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitia ubani kuashiria kuaza kwa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana usiku 18-10-2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akitia ubani wakati wa hafla ya Maulidi ya kusherehekea Kuzaliwa kwa Mtume Muhammed (S.A.W) yaliyofanyika jana usiku 18-10-2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na (kulia kwake) Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Zuhura Kassim Ali na (kushoto kwake) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Sharifa Omar Khalfan.(Picha na Ikulu)

WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakijumuika katika hafla ya Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika jana usiki 18-10-2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman, Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)

USTADHI Hamdan Haji Hamdan kutoka Magogoni Wilaya ya Magharibi “B”Unguja, akisoma Quran Sura An Aam aya 44-48, kabla ya kuaza kwa Maulid ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 18-10-2021.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akihudhuria Maulid ya kusherehekea Maulid ya Kuzaliwa kwa Mtume Mohammad (S.A.W) yaliyofanyika katika Uwanja wa Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja na (kulia kwake) Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zuhura Kassim Ali na (kushoto kwake) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa 0mar Khalfan.(Picha na Ikulu)

WAGENI waalikwa Masheikh kutoka Nchini Misri walioko Zanzibar wakishiriki katika hafla ya sherehe za Maulidi ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika uwanja wa Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku,18-10-2021.(Picha na Ikulu)

WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakijumuika katika hafla ya Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika jana usiki 18-10-2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman, Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)

USTADH Khamis Ali Adam kutoka Bumbwini Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja akisoma Maulid ya Barzanji Mlango wa kwanza, katika hafla ya Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika jana usiku 18-10-2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar katika hafla ya kusherehekea Maulidi ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika katika Uwanja wa Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 18-10-2021, na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzaibar Sheikh. Saleh Omar Kabi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj. Othman Masoud Othman.(Picha na Ikulu)

USTADH.Nassor Seif Rashid kutoka Kibanda Hatari Wilaya ya Mjini Unguja akisoma Maulid ya Barzanji Mlango wa Nne wenye kisimamo na Sala ya Mtume Muhammad .S.A.W, wakati wa Maulid ya kusherehekea Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad S.A.W yaliofanyika jana usiku 18-1-2021 katika viwanja vya Maisara Suleiman.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa katika kisimamo cha Qiyaam na kumsalia Mtume Muhammad SAW, wakati wa hafla ya Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika jana usiku katika uwanja wa Maisara Suleiman na ( kulia kwake) Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Zuhura Kassim Ali na ( kushoto kwake) Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Sharifa Omar Khalfan na Mke wa Makamu wa Kwanza Mama Zainab Kombo Shaib.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika kisimamo cha Qiyaam na kumsalia Mtume Muhammad (S.A.W) katika Maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.AW) yaliofanyika katika viwanja vya Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja jana usiku 18-10-2021, na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sheria,Katiba,Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla .(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Qasweeda ya Mwaka wa Kiislam Al Hijra 1443 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Milade Nabii Association Zanzibar Bw. Sherali Champsi, wakati wa sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliofanyika jana usiku katika uwanja wa Maisara Suleiman Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments