Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI DKT MABULA ATEMBELEA TIMU YA WIZARA YA ARDHI INAYOSHIRIKI MICHUANO YA SHIMIWI MOROGORO

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wachezaji wa timu ya Wizara ya Ardhi inayoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) alipoitembelea kambi ya timu hiyo iliyoko Mazimbu mkoani Morogoro tarehe 28 Oktoba 2021.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Wizara ya Ardhi inayoshiriki michuano ya Shirikisho la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) alipotembelea kambi ya timu hiyo iliyoko Mazimbu mkoani Morogoro tarehe 28 Oktoba 2021.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya mpira wa Pete (Netball) ya Wizara ya Ardhi inayoshiriki mashindano ya Shirikisho la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) alipoitembelea kambi ya timu hiyo Mazimbu mkoani Morogoro tarehe 28 Oktoba 2021.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Ardhi inayoshiriki michuano ya Shirikisho la Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) alipoitembelea kambi ya timu hiyo iliyopo Mazimbu mkoani Morogoro tarehe 28 Oktoba 2021.


*****************************

Na Munir Shemweta, WANMM MOROGORO


Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ametembelea kambi ya Timu ya Wizara ya Ardhi iliyoko Mazimbu mkoani Morogoro kwa lengo la kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo wanaoshiriki Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI).

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mashindano hayo inawakilishwa na timu mbili za mpira wa miguu na mpira wa pete (Netball) na timu hizo zimeanza kufanya vizuri katika michezo yake ya awali.

Katika michezo yake ya awali timu ya mpira wa miguu ya Wizara ya Ardhi Ilizifunga timu za Katiba 1-0 na TARURA magoli 3-0 wakati timu ya mpira wa pete ikiifunga Uchukuzi kwa point 14-13 na Kilimo 23-12 na kutoka sare ya 23-23 na NFRA

Akizungumza na wachezaji wa timu hizo tarehe 28 Oktoba 2021 mkoani Morogoro, Naibu Waziri Dkt Mabula aliwataka wachezaji wa timu hizo kujituma na kuwa na nidhamu katika kipindi chote cha mashindano ili waweze kupata ushindi na hatimaye kurudi na vikombe.

‘’ Cha kuzingatia wakati wa kushiriki mashindano haya ya SHIMIWI ni kuwa na nidhamu pamoja na kujituma ili muweze kuibuka washindi katika mechi zenu na hatimaye mrudi na vikombe’’ alisema Naibu Waziri Mabula.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mbali na michuano ya SHIMIWI kushindanisha Wizara na Idara za Serikali kwa lengo la kupata washindi lakini michuano hiyo inasaidia kuimarisha afya za watumishi na wakati huo kujenga mahusiano baina ya watumishi.


Post a Comment

0 Comments