*****************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Barcelona imemtimua kocha wao Rinald Koeman mara baada ya muendelezo wa matokeo mabaya tokea msimu huu kuanza.
Usiku wa kuamkia jana Barcelona imepokea kichapo kutoka kwa Rayo Vollacano kwa bao 1-0 na kuwafanya kushika nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Ligi.
Makocha kadhaa wametajwa kuchukua mikoba ya Mholanzi huyo huku Xavi Hernandez akiwa mmoja wa makocha hao watakao chukua nafasi hiyo.
Katika msimamo wa La Liga mpaka sasa Real Madrid wanaongoza wakiwa wamecheza michezo 10 na kujinyakulia pointi 21.
0 Comments