Afisa Mhifadhi Msaidizi Bw.Allan Mushi akimshikisha fuvu la mnyama swala mwandishi wa habari wa ITV Mkoa wa Morogoro Bi.Hilda Mushi mara baada waandishi Mkoa huo kutembelea Hifadhi yya Taifa ya Mikumi hapo jana.
Afisa Mhifadhi Msaidizi Bw.Allan Mushi akiwashiikisha fuvu la mnyama swala waandishi wa habari wa ITV Mkoa wa Morogoro Bi.Hilda Mushi mara baada waandishi Mkoa huo kutembelea Hifadhi yya Taifa ya Mikumi hapo jana. Afisa Mhifadhi Msaidizi Bw.Allan Mushi (Katikati) akipata picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Morogoro mara baada yya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi jana.
Baadhi ya Tembo wakiwa katika Hifadhi ya Taifa Mikumi.Tembo wamekuwa wakipatikana kwa wingi katika hifadhi hiyo pia ni kutokana na usalama wao.Baadhi ya Pundamilia wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.Pundamilia wamekuwa wakipatikana kwa wingi katika hifadhi hiyo ambapo wanapatikana katika maeneo mbalimbali yya malisho kwenye hifadhi hiyo.
Baadhi ya wageni wakiwasili katika uwanja wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Taifa Mikumi kwaajili ya Utalii kwenye hifadhi hiyo. Baadhi ya wageni wakiwasili kwa njia ya gari katika geti la kuingilia Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwaajili ya kutalii.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, MIKUMI
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi licha ya kusifika kuwa na wanyama wengi kumekuwa na utalii wa kutembea kwa miguu (Walking) ambapo inamsaidia mtalii kuona na kujifunza mambo mengi kwa uhalisia.
Akizungumza katika hifadhi hiyo Afisa Mhifadhi Msaidizi Bw.Allan Mushi amesema kuna umuhimu wa watalii kutalii kwa kutembea kwa miguu katika hifadhi kwani ni rahisi kwake kutambua na kuona mambo mengi yaliyopo kwenye hifadhi.
"Ukiwa unafanya utalii wa kutembea kwa miguu kuna vitu vingi vya kujjifunza mfano, kuna nyao za wanyama, kinyesi cha wanyama na hata muda mwingine kutambua tabia za wanyama". Amesema Bw.Mushi.
Aidha Bw.Mushi amesema kuna muda unaweza ukatambua muda ambao wanyama wamepita katika eneo fulani kwa kutazama unyayo wa miguu pamoja na kinyesi cha mnyama katika eneo fulani.
Amesema kabla ya zoezi la kutalii kwa kutembea kwa miguu hutoa elimu kwanza kwa watalii pindi kukitokea kwa mnyama mkali mbele yao wawezee kufanya nini ili asiweze kudhurika.
Pamoja na hayo Bw.Mushi amesema katika zoezi la kutalii kwa kutembea kwa miguu usalama huwa upo kwani lazima kuwepo kwa askari wenye silaha wakiwaongoza watalii katika maeneo ambayo kuna wanyama.
0 Comments