*****************************
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ta Rais TAMISEMi Dkt. Grace Magembe amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Mhe. Meja Edward Gowele kwa kutekeleza maelekezo ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI yaliyowataka viongozi wote kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya na Halmashauri kushiriki kwenye ukaguzi wa bidhaa za Afya (Health Commodities Audit) badala ya kuwaachia wataalamu wa Afya peke yao.
Dkt. Grace ametoa pongezi hizo baada ya Meja Gowele kubaini uchepushaji wa dawa katika Hospital ya Wilaya ya Rufiji na kufuatilia mpaka kuhakikisha dawa hizo zimepatikana na zimerejeshwa Hospitalini.
Amewataka viongozi wengine kuiga mfano huu na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika ukaguzi wa bidhaa za Afya ili bidhaa hizo ziweze kuwafikia walengwa ambao ni wananchi.
Pia amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuchunguza tukio hilo na kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo.
Wakati huo huo Dkt. Grace amewataka wananchi kutoa taarifa kwa viongozi mara wanapobaini au kupata fununu za matumizi mabaya ya rasilimali za Serikali kwenye Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
0 Comments