Ticker

6/recent/ticker-posts

BILIONI 3 ZAKAMILISHA MRADI WA MAJI KIRANDO KAMWANDA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti (kulia) akiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa SUWASA Mhandisi Gibon Nzowa wakati alipokagua mradi wa maji wa Kirando Kamwanda wilayani Nkasi juzi.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti akiongea na mafundi kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa maji Kirando wilaya ya Nkasi juzi ambapo amewasihi kuzingatia viwango vya ubora ili unufaishe wananchi wengi na kwa kipindi kirefu.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Kirando iliyopo wilaya ya Nkasi juzi ambapo ameahidi kusaidia kupatikana walimu wa masomo ya sayansi.
Mafundi wa shirika la ugavi wa umeme (Tanesco) wakiendelea na kazi ya kufunga transfoma itakayotumika kwenye mradi wa maji wa Kirando Kamwanda uliopo mwambao wa Ziwa Tanganyika wilaya ya Nkasi . Tenki jipya la kuhifadhia maji lenye uwezo wa lita milioni lililokamilika kujengwa kwenye mradi wa Kirando Kamwanda wilaya ya Nkasi chini ya SUWASA ambapo mradi huo utahudumia wananchi wapato 74,000 wa vijiji saba.


(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)




***************************



Wananchi 74,483 wa vijiji saba vilivyopo mwambao wa Ziwa Tanganyika katika tarafa ya Kirando wilaya ya Nkasi watanufaika na upatikanaji maji safi na salama kufuatia serikali kukamilisha mradi wa Kirando Kamwanda..

Hayo yamebainishwa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Sumbawanga (SUWASA) Mhandisi Gibon Nzowa wakati Akiwasilisha taarifa ya mradi huo kwenye ziara ya mkuu wa mkoa iliyofanyika eneo la mradi kijiji cha Kirando.

“Mradi huu wa Kirando Kamwanda umesanifiwa ili kufikia watu 74,483 wa tarafa ya Kirando ambapo jumla ya shilingi Bilioni 3.1 zimetumika kwenye utekelezaji wa mardi huu uliofikiwa asilimia 90 hadi sasa” alisema Mhandisi Nzowa.

Nzowa alitaja kazi zilizkmilika kuwa ni ujenzi wa Chanzo toka Ziwa Tanganyika, ujenzi wa nia kuu ya bomba mita 433, ujenzi wa tanki jipya la kuhifadhia maji lenye lita Milioni moja na ujenzi wa njia ya matandao wa usambazaji maji wenye urefu wa kilometa 26.8

Akizungumza na wananchi wa Kirando kwenye mkutano wa hadhara ,Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joseph Mkirikiti aliwasihi watunze vyanzo vya maji na miundombinu ili mradi huo udumu vizazi vingi vijavyo

Mkirikiri aliongeza kusema ni jukumu la kamati ya watumie maji Kirando kuweka utaratibu wa kuchangia fedha kidogo kwa ajili ya kuendesha mradi huo kwa kuwa serikali itapenda kuona fedha iliyotumika ikirudi kwa njia ya kutunza mradi huo .

“Gharama ya utekelezaji mradi huu wa maji haiendani na kiasi cha fedha kitakachorudi baada ya mradi kuanza, hivyo tunataka wananchi kupitia jumuiya ya watumie maji kuwa na utaratibu wa kuchangia fedha za kufanyia ukarabati pale miundombinu itakapoharibika” alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kirando Kakuri Seba aliipongeza serikali kwa kukamilisha mradi huu ambao ulianza muda mrefu ambapo awali ulikabiliwa na ukosefu wa fedha lakini serikali ya awamu ya Tano imekamilisha kwa kutoa fedha.

Kiongozi huyo wa kata alimhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa ataendelea kuhamasisha wananchi kuutunza mradi huo wa maji ikiwemo miundombinu yake iwe endelevu.

Kwa mujibu wa taarifa ya SUWASA mradi utahudumia vijiji saba vya wilaya ya Nkasi ambavyo ni Kamwanda, Mtakuja, Kichangani, Itete, Chongokatete, Shaurimoyo na Isasa.

Post a Comment

0 Comments