Ticker

6/recent/ticker-posts

WAJUMBE WA KAMATI YA MTAKUWWA WATAKIWA KUSIMAMIA VYEMA UTEKELEZAJI WA MPANGO KAZI WA TAIFA WA KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO



Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kasper Mmuya akizungumza na Wajumbe wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto wakati wa ziara yake ya Kikazi kwa lengo la ufuatilia utekelezaji wa afua mbalimbali za Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Wadau Mkoani Shinyanga.


Wajumbe wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto wakisikiliza maelezo ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kasper Mmuya alipotembelea Ofisi ya Halimashauri ya Kahama kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa afua za MTAKUWWA.


Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Kahama Robert Kwela akieleza jambo wakati wa ziara hiyo ya Naibu Katibu Mkuu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa afua za MTAKUWWA. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kasper Mmuya.


Mratibu wa Taifa wa Mpango wa MTAKUWWA Bi. Happiness Mugyabuso akieleza jambo wakati wa kikao kilichokuwa kikiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa afua za MTAKUWWA.


Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Halmashauri ya Kahama, Abrahaman Nuru (kushoto) akimuonyesha Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kasper Mmuya (kulia) mfumo wa kuhifadhia taarifa za waanga wa vitendo vya ukatili.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kasper Mmuya (kulia) akiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na mabinti na Mama wadogo wanaojishughulisha na ujasiriamali kupitia miradi inayotekelezwa na wadau ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo wa kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi yao na mazingira hatarishi.

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU

(SERA, URATIBU, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)

********************************

Na: Mwandishi Wetu, Kahama

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kasper Mmuya amewataka Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata na Kijiji/Mtaa kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ili kujenga jamii bora yenye usawa.

Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu huyo wakati wa ziara yake ya Kikazi Mkoani Shinyanga kwa lengo la ufuatilia utekelezaji wa afua mbalimbali za Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) zinazotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Wadau mkoani humo.

Naibu Katibu Mkuu Mmuya alisema kuwa kama Taifa Serikali kwa kushirikiana na wadau waliandaa mpango kazi huo wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) ili kukabiliana na changamoto za ulinzi zinazowakabili wanawake na watoto nchini, hivyo katika kutekeleza mpango huo kwa ufanisi ni vyema Wajumbe wa Kamati ya MTAKUWWA kuanzia ngazi Kitaifa na ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata na Kijiji/Mtaa kuhakikisha wanasimamia vyema utekelezaji wa Mpango Kazi huo.

“Katika kusimamia vyema mpango kazi huu ni muhimu kila mjumbe akutambua eneo lake la utekelezeaji ili kila mdau anayehusika katika masuala ya kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wakawa na uelewa wa pamoja wa mpango kazi huo wa Taifa ili waweze kuzingatia usimamizi wa MTAKUWWA kwa kuwashirikisha wadau katika kutekeleza mpango kazi wa Taifa wa MTAKUWWA,” alisema Mmuya

Alifafanua maeneo hayo ya utekelezaji yaliyopo katika mpango kazi huo ambayo ni Kuimarisha Uchumi wa kaya; Mila na Desturi; Mazingira salama; Malezi, kuimarisha mahusiano na kuziwezesha familia; Utekelezaji na usimamizi wa Sheria; Utoaji huduma kwa waathirika wa ukatili; mazingira salama shuleni na stadi za maisha; na Uratibu, Ufuatiliaji na Tathmini.

Sambamba na hayo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kasper Mmuya alipongeza Wilaya ya Kahama na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla kwa namna wanavyotekeleza afua mbalimbali za MTAKUWWA katika kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

Aidha Naibu Katibu Mkuu Mmuya alitoa wito kwa Maafisa Ustawi wa Jamii kuimarisha ushirikiano na wadau katika kutekeleza kutekeleza afua mbalimbali za MTAKUWWA katika kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

“Mkoa wa Shinyanga mnafanya vizuri katika kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia na Watoto kupitia mpango mkakati wa mkoa ambao umekuwa chachu ya mabadiliko hayo. Niwapongeze pia wadau mmekuwa na ushirikiano mzuri na serikali,” alisema Naibu Katibu Mkuu Mmuya

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga alisema kuwa Halmashauri hiyo imekuwa ikipambana kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na Watoto kwa kuhakikisha kila mdau na mratibu anatimiza wajiubu wake kwa ufanisi.

Akitoa neno la shukrani kwa Serikali Mmoja wa wanakikundi cha The Best Mwajuma Ramadhani ameishukuru serikali kwa kutambua wadau ambao wamekuwa na msaada mkubwa na unaowafikia moja kwa moja mabinti na waototo ambao wamekuwa wakiishi katika mazingira hatarishi.

“Wadau hawa wameweza kutujengea uwezo ambao hii leo tunauwezo wa kuanzisha biashara na shughuli ambazo zimetufanya tuondokane katika mazingira ya utegemezi kwa familia zetu sambamba na kuwa na ujasiri wa kutekeleza vitu kwa vitendo,” alisema Mwajuma

Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kasper Mmuya alitembelea Mahakama, Madawati ya Jinsia katika Vituo vya Polisi, Kituo cha Mkono kwa Mkono (One Stop Center) cha Shufa kinachotoa huduma jumuishi kwa waathirika wa ukatili. Aidha alitembelea shughuli za ujasiriamali zinazofanywa na mabinti na Mama wadogo waliopo chini ya miradi inayotekelezwa na wadau mbalimbali. Pia alikutana na kuzungumza na Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto.

Post a Comment

0 Comments