Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Mhe. Dmytro Senik (hayupo pichani) yaliyofanyika leo Septemba 22, 2021.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Mhe. Dmytro Senik wakiwa katika mazungumzo.
Mazungumzo yakiendelea
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akifuatalia mazungumzo.
*********************************
Ukraine imeeleza kuwa Oktoba, 2021 inatarajia kufungua kituo chake cha kushughulikia VISA kwa Watanzania wanaosafiri kwenda nchini humo kwa shughuli mbalimbali. Hatua hii inalenga kuwaondolea usumbufu Watanzania wanaosafiriki kwenda nchini humo ambapo kwa sasa wanalazimika kwenda jijini Nairobi, Kenya kushugulikia VISA za safari zao.
Haya yameelezwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ambaye mapema leo alifanya mazunguzo kwa njia ya Mtandao na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Mhe. Dmytro Senik.
Balozi Mbarouk ameongeza kuwa katika mazumgumzo hayo pia wamejadili namna ya kushirikiana katika maeneo ya Biashara na Uwekezaji, Kilimo, Elimu na Viwanda. Katika eneo la kilimo Naibu Waziri Senik ameleza kuwa Ukuraine ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kilimo cha ngano ili kuongeza uzalishaji na ubora wa zao hilo. Vilevile Waziri Senik ameeleza utayari wa Ukraine kusaini makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya ya elimu na Tanzania.
Aidha, Naibu Waziri Senik ameeleza kuwa siku za usoni anatarajia kuja nchini Tanzania ambapo ataambatana na ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji wa nchini Ukraine kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara.
Julai 2021, Tanzania na Ukraine zimetimiza miaka 29 ya mahusiano ya kidiplomasia ambapo zimeendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara na elimu. Mathalani idadi ya watalii wanaotembelea nchini kutoka Ukraine imeongezeka kutoka watalii 1352 kwa mwaka 2014 hadi 7260 kwa mwaka 2020.
0 Comments