Ticker

6/recent/ticker-posts

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHENJUA MADINI YA BATI WILAYANI KYERWA.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ameshika mawe yenye madini ya Bati wakati alipokagua mitambo ya kampuni ya kuchenjua madini ya Bati ya African Top Minerals iliyopo Kyerwa Mkoani Kagera, Septemba 20 2021. Kulia ni Mhasibu wa Kampuni hiyo, Hamisi Kohomin . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Hamisi Kohomin ambaye ni Mhasibu wa Kampuni ya kuchenjua madini ya Bati ya African Top Minerals ya Kyerwa Mkoani Kagera, Septemba 20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakishuhudia wakati Hamis Kohomin ambaye ni Mhasibu wa kampuni ya kuchenjua madini ya Bati ya African Top Minerals ya wilayani Kyerwa alipowaonesha namna ya kupima ubora wa madini hayo, Septemba 20, 2021. Mheshimiwa Majaliwa yuko Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipata maelezo kuhusu madini ya Bati kutoka kwa Hamisi Kohomin ambaye ni Mhasibu wa Kampuni ya Kuchenjua Madini ya African Top Minerals ya Kyerwa Mkoani Kagera wakati Waziri Mkuu alipokagua mitambo ya kampuni hiyo, Septemba 20, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa kampuni ya kuchenjua mkadini ya Bati (TIN) ya African Top Minerals baada ya Waziri Mkuu kukagua mitambo ya kampuni hiyo wilayani Kyerwa, Kagera, Septemba 20, 2021. Wa tano kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


***************************************



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 20, 2021 ametembelea na kukagua kiwanda cha kuchenjua madini ya bati (TIN) cha kampuni ya African Top Minerals kilichopo wilayani Kyerwa ambapo alitumia fursa hiyo kumuhakikishia mwekezaji huyo kwamba Serikali itaendelea kumuunga mkono.

Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Hassan Ibar alisema mradi huo uliogharimu shilingi bilioni nne unalengo la kuboresha na kukuza sekta ya madini wilayani Kyerwa na Tanzania kwa kuongeza thamani ya madini hayo katika soko la dunia, hivyo kuongeza kipato kwa wananchi.

Aliishukuru Serikali kwa jitihada zake za kutambua mchango wa madini ya bati kwa kuzindua cheti cha uhalisia cha madini hayo ambacho kimewasaidia kutambulika kimataifa na kufanya biashara yao kwa uhakika.

“Tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Samia kwa jitihada zake za kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wawekezaji, tutaendelea kumuunga mkono.”

Post a Comment

0 Comments