*********************
Na.WAMJW-IRINGA
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa imetakiwa kukamilisha ujenzi wa Jengo la huduma za wagonjwa mahututi na dharura ifilapo mwezi November Mwaka huu.
Hayo yamesemwa Leo na Katibu MKUU wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Hapa
Prof. Makubi amesema ujenzi huo unatakiwa umalizike ili lianze kutoa huduma ifikapo mwezi Novemba 2021.
"Hongereni kwa kukaribia kumaliza hili jengo na sasa mkamilishe hatua za mwisho ili huduma zianze kutolewa Novemba 2021, aliseema Prof Abel Makubi,
Aliongeza kuwa Kumalizika kwa Jengo hilo la Wagonjwa mahututi na dharua , ni matokeo ya juhudi za Serikali ya awamu ya chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, na limegharimu shillingi milioni 600.
Prof. Abel Makubi pia alitembelea Maabara, wodi za wagonjwa na huduma za nje (OPD) ,na kuongea na Wananchi kuhusu Kampeni za kutekeleza mpango wa Jamii Shirikishi na harakishi wa kuhamasisha Wananchi kuchanja katika halmashauri mbalimbali nchini.
0 Comments