Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Ushirika yaliyofanyika katika ukumbi wa BOT mkoani Mtwara, jana. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda pamoja na Naibu Waziri, Hussein Bashe wakiwa wameongozana na viongozi wengine wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakikagua maghala yaliyopo katika bandari ya Mtwara kuelekea kuanza msimu wa uuzwaji wa korosho ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni wakati wa ziara ya Waziri Mkenda bandarini hapo, Tarehe 20 Septemba 2021.

Waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda pamoja na Naibu Waziri, Hussein Bashe wakiwa wameongozana na viongozi wengine wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakikagua utayari wa bandari ya Mtwara kuelekea kuanza msimu wa uuzwaji wa korosho ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni wakati wa ziara ya Waziri Mkenda bandarini hapo, tarehe 20 Septemba 2021.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
WAZIRI wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda amesema Bandari ya Mtwara imejiandaa vizuri kwa ajili ya kusafirisha zao la korosho na uamuzi huo hautabadilika kwa kuwa ni maekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha, amepiga marufuku matumizi ya kangomba kwenye mauzo ya zao hilo huku akieleza kufanya hivyo kutachelewesha kuuzwa kwa bei nzuri na watu kuandaa mashamba kwa wakati.
Hayo ameyasema mjini Mtwara wakati alipotembelea bandari hiyo kwa lengo la kuangalia kama maelekezo ya Rais kuhusu korosho yote kusafirishwa kupitia hapo yametekelezwa.
“Haya ni maelekezo ya serikali kwamba korosho yote huku itapitia bandari hii maagizo hayo ni ya Rais hayatabadilika kwa hiyo wote ambao wanataka kufanya biashara ya Korosho wajipange “
“Zaidi ya hapo hapa bandarini wanafanya kazi saa 24 kwa hiyo meli ikija kama ni kupakia inapakia kwa muda na kasi sana kwa sababu ya uwezo huo wa kufanya kazi muda wote,” amesema.
Amesema kuwa Serikali imeshatoa kibali wanaosafirisha korosho kuleta bandari ya Mtwara wanaruhusiwa kufanya hivyo kwa saa 24 hivyo wameshatengua kanuni zilizokuwa zinaeleza baada ya saa 12 huwezi kusafirisha zao hilo.
Amesisitiza kuwa mtu akitaka kununua korosho lazima apitishe kwenye Bandari hiyo kwakuwa gharama zimepunguzwa hivyo kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kusafirisha kwa njia nyingine.
“Tunasisitiza si kwa sababu tunataka bandari hii ifanye kazi bali uzoefu unaonyesha kwamba korosho inaponunuliwa kutoka Mtwara yenye ubora inaposafirishwa mpaka Dar es Salaam baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakiiharibu kwa kuongeza vitu au kuweka isiyofaa.
Katika hatua nyingine amepiga marufuku matumizi ya kangomba huku akieleza kwa kufanya hivyo kutachelewesha kuuza kwa bei nzuri bidhaa hiyo na watu kuandaa mashamba kwa wakati.
Naibu Waziri wa kilimo, Hussein Bashe amesema wataendelea kufanya kazi na mamlaka ya Bandari na kupitia kikao kitakachofanyika Alhamisi jijini Dar es Salaam watajadili hoja mbalimbali zilizotolewa na wasafirishaji wa zao hilo.
Amezitaja baadhi ya hoja hizo ni gharama ya uhifadhi, upatikanaji wa makasha, muda wa kuhifadhi makasha ya wasafirishaji ambao kwa sasa umeongezwa kutoka siku 14 mpaka 21, uwezo uliopo ni kuhifadhi makasha 13000 kwa wakati mmoja hivyo hakuna tatizo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Karim Mattaka amesema wapo tayari kuhudumia shehena hiyo kwa kuwa wameongeza uwezo wa kuhifadhi na kuhudumia korosho kwa kuongeza eneo na vifaa.
MWISHO
0 Comments