Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Charles Mkombe akizungumza wakati wa semina hiyo
MWAKILISHI wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi kutoka Dodoma Mwita Waibe akizungumza wakati wa semina elekezi kwa watumishi wa Afya Jijini Tanga na waandishi wa Habari kuhusu Ugonjwa wa Covid 19 iliyofanyika Jijini Tanga kulia ni Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga Charles Mkobe
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
MGANGA Mkuu wa Jiji la Tanga (CMO) Dkt Charles Mkombe amesema kwa mujibu wa takwimu zao mpaka Septemba 27 mwaka huu walikuwa wamechanga chanjo ya Uviko watu 6000.
Mkombe aliyasema hayo wakati wa semina elekezi kwa watumishi wa Afya Jijini Tanga na waandishi wa Habari kuhusu Ugonjwa wa Covid 19 iliyofanyika Jijini Tanga
Alisema kampeni ya Kitaifa ya kuharakisha utoaji wa chanjo ya uviko 19 itasaidia kutokana na kama dunia imekumbwa na janga kubwa na lina madhara makubwa na watu wengi wameungua korona na wengine wamefariki.
Aidha alisema ugonjwa huo umeleta changamoto ya matumizi ya dawa na vifaa tiba na ya kiuchumi maana kabla ya Korona watu walikuwa wanafanya biashara vizuri lakini sasa zimefungwa.
“Madhara ya Korona ni zaidi ya kiafya imegusa ishu za kijamii na kiuchumi na kumekuwa na ongezeo la gharama za vitu mbalimbali ikiwemo vifaa vya hospitali gharama zimepanda mara dufu”Alisema
Alisema ugonjwa huo umeleta mtikisiko mkubwa kwenye jamii na watu wamekata tamaa wamekuwa ni waoga kuishi
Awali akizungumza Afisa Afya wa Mkoa wa Tanga Magoma alisema mkoa huo chanjo ya Uviko 19 ilikuwa inasua walipokea dozi 35000 na walianza rasmi Agosti 3 mwaka huu na ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo Adam Malima ilikuwa ya kusuasua kidogo kutokana na vituo vilivyofunguliwa kuwa vichache .
Alisema wana vituo zaidi ya 300 na vituo ambavyo vilikuwa vinatoa huduma ni 33 huku vituo vitatu kila Halmashauri na baadhi ya maeneo mengine kutoka kituo hadi wananchi walipo inabidi watembee umbali mrefu au wakalale huko karibu na vituo vya jiriani.
“Lakini pia kuchelewa kufikia lengo la uchanjaji na tuna lengo la kutazama mabadiliko walizopewa kumaliza kwenye muda uliowekwa”Alisema
Hata hivyo alisema sababu kubwa ni vituo kuwa mbalimbali na wananchi Lakini suala hilo limefanyiwa kazi na halmashauri hivi sasa zimefungua kliniki za mkoba lakini vituo vinavyotoa bila kujali vya serikali,vya umma au madhehebu ya dini vitakuwa vinatoa chanjo na elimu inaendelea kwa jamii ili kuona umuhimu wa chanjo kuweza kudhibiti ugoinjwa wa Uviko.
Hata hivyo kwa upande wake Mwakilishi wa Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi kutoka Dodoma Mwita Waibe amesema hivi sasa Taifa litaendelea kutoa chanjo ya Uviko 19 kwa wananchi wake ili wasiendelee kupata madhara yatokanayo na ugonjwa huo.
Waibe Mwita ambaye pia ni Mkuu wa Msafara uliopo Tanga kuhamasisha suala la chanjo ya UVIKO 19 kwa mkoa wa Tanga Mwita Waibe ambapo alisema madhara hayo ni yaliyojitokeza huko nyuma wakati chanjo haikuwepo.
Alisema Taifa limejiridhisha kwamba chanjo hizo ni salama na hazina madhara ya aina yoyote hivyo wananchi wahakikisha wanajitokeza kupata chanjo hizo.
Aidha alisema wanaendelea kuangalia hali upokeaji umekuwaje na changamoto kubwa kutokana na kwamba mikoa inatofautiana kwa hiyo katika ngazi ya Taifa ikaona ni vizuri kuwafikia wananchi kuanzisha zoezi la kushawisha kuharakisha uhamamsisha kwa wananchi ili waweze kupata uelewa
Alisema wataendelea kufanya utafiti kama serikali kuona uchukuaji wa chanjo na upokeaji baada muda wanakaona kuna changamoto kubwa ni suala pamoja wapo ni upatikanaji wa chanjo karibu na wananchi na elimu ni changamoto hayo ndio maana wameamua kutengeneza kampeni harakishi kuhakikisha wananchi wanapewa elimu.
“Lakini kuhakikisha chanzo zote zilizokuwa zikitolewa kwenye vituo vichache zinatolewa kwenye vituo vyote vya kutoa huduma ya afya”Alisema
Awali akizungumza Afisa Afya wa Mkoa wa Tanga Magoma alisema mkoa huo chanjo ya Uviko 19 ilikuwa inasua walipokea dozi 35000 na walianza rasmi Agosti 3 mwaka huu na ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa huo Adam Malima ilikuwa ya kusuasua kidogo kutokana na vituo vilivyofunguliwa kuwa vichache .
Alisema wana vituo zaidi ya 300 na vituo ambavyo vilikuwa vinatoa huduma ni 33 huku vituo vitatu kila Halmashauri na baadhi ya maeneo mengine kutoka kituo hadi wananchi walipo inabidi watembee umbali mrefu au wakalale huko karibu na vituo vya jiriani.
“Lakini pia kuchelewa kufikia lengo la uchanjaji na tuna lengo la kutazama mabadiliko walizopewa kumaliza kwenye muda uliowekwa”Alisema
Hata hivyo alisema sababu kubwa ni vituo kuwa mbalimbali na wananchi Lakini suala hilo limefanyiwa kazi na halmashauri hivi sasa zimefungua kliniki za mkoba lakini vituo vinavyotoa bila kujali vya serikali,vya umma au madhehebu ya dini vitakuwa vinatoa chanjo na elimu inaendelea kwa jamii ili kuona umuhimu wa chanjo kuweza kudhibiti ugonjwa wa Uviko.
0 Comments