NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) katika Mikoa 20 tayari imesajili watoto walio chini ya miaka 5 zaidi ya Milioni Sita na kufikia asilimia 55% kutoka asilimia 13% mwaka 2012 kupitia mpango mkakati wa usajili aliouzindua mwaka 2018 na kutoa matokeo chanya kwa sehemu nyingi nchini kusajili watoto wengi ikiwemo mikoa ya Mara na Simiyu ambayo ndani ya miezi minne ilisajili watoto na kufikia asilimia 80% kutoka asilimia 10% za awali.
Ameyasema hayo leo Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi wakati wa maadhimisho ya nne ya Siku ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Barani Afrika yanayoadhimishwa Agosti 10 kila mwaka.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Prof. Kabudi amesema zoezi la usajili linalofanywa na RITA ni muhimu na hufanyika kote nchini ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango ya kuwahudumia wananchi na imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali na kuleta matokeo makubwa ambayo pia yanategemewa kupatikana kupitia sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka ujao.
Aidha amesema mpango wa Usajili wa vifo ambao unatekelezwa sambamba na usajili wa watoto utasaidia kutambua idadi ya vifo vinavyotokea nchini sababu za vifo pamoja na kuboresha huduma za Afya sehemu mbalimbali na kuitaka wakala hiyo kutoa elimu zaidi kwa jamii kuhusu umuhimu wa uwekaji wa takwimu za matukio muhimu ya Binadamu ya vifo, vizazi, ndoa na watoto wa kuasili.
"licha kuwepo na changamoto ya janga la UVIKO-19, RITA imepiga hatua kubwa hasa katika matumizi ya teknolojia katika utoaji huduma ambapo hadi sasa huduma nyingi zinazotolewa na RITA zinatolewa kwa njia ya mtandao wa simu ikiwemo huduma za usajili wa vizazi na vifo kwa kukamilisha maombi kwa njia ya kieletroniki bila kufika katika ofisi zao". Amesema Prof.Kabudi.
Sambamba na hayo Prof. Kabudi amesema katika suala la ndoa sio kila kiongozi wa dini anaruhusiwa kufungisha ndoa kwani kisheria ni mpaka kiongozi huyo awe amesajiliwa na RITA tofauti na hapo ndoa hiyo ni batili.
Aidha amewaomba viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu waliohudhuria katika semina hiyo kuhakikisha kuwa wanatoa maoni ambayo yataboresha haki za watu wenye ulemavu na kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi wa Haki za Kisheria RITA Lina Msanga amesema maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila Agosti 10 barani Afrika yanalenga kuongeza mwamko na kasi ya wananchi ya kusajili matukio muhimu na yanafaa kupewa kipaombele kwani yanasaidia nchini kufanya mambo ya maendeleo.
Hata hivyo amesema kauli mbio ya maadhimisho hayo ni uongozi kwa huduma muhimu kujenga mifumo imara ya usajili wa matukio muhimu ya Binadamu Afrika inayowezesha ubunifu jumuishi na inayogatua utoaji wa huduma baada ya kipindi cha Covid 19 ambayo inatekelezwa na Umoja wa Afrika (AU) kwa nchi zote Barani Afrika.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya nne ya Siku ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Barani Afrika yanayoadhimishwa Agosti 10 kila mwaka.Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya RITA, Bw.Khamis Duhenga akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya nne ya Siku ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Barani Afrika yanayoadhimishwa Agosti 10 kila mwaka.Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam. Mwenyekiti wa shirikisho la vyama la watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA,) Bi.Tulia Mwantala akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya nne ya Siku ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Barani Afrika yanayoadhimishwa Agosti 10 kila mwaka.Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Ulinzi wa Haki za Kisheria RITA, Bi. Lina Msanga akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya nne ya Siku ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Barani Afrika yanayoadhimishwa Agosti 10 kila mwaka.Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia Maadhimisho ya nne ya Siku ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Barani Afrika yanayoadhimishwa Agosti 10 kila mwaka.Hafla hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
0 Comments