Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene,akizungumza akifungua kongamano la wanawake waombolezao kitaifa kwa ajili ya maombi ya kuiombea mihimili ya Mahakama, Bunge na Serikali lililofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kongamano la wanawake Dk. Juliana Manyerere,akizungumza wakati wa akongamano la wanawake waombolezao kitaifa kwa ajili ya maombi ya kuiombea mihimili ya Mahakama, Bunge na Serikali lililofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma.
Washiriki wa Kongamano wakifatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene,(hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la wanawake waombolezao kitaifa kwa ajili ya maombi ya kuiombea mihimili ya Mahakama, Bunge na Serikali lililofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene,akifanyiwa maombi mara baada ya kufungua kongamano la wanawake waombolezao kitaifa kwa ajili ya maombi ya kuiombea mihimili ya Mahakama, Bunge na Serikali lililofanyika leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma.
..........................................................................
Na. Benedict Mwasapi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amewataka wanawake wote nchini kusimama kama mama katika familia zao kuliombea Taifa hususani linapokuwa katika kipindi kigumu cha kukabiliwa na majanga mbalimbali ya dunia.
Hayo ameyasema leo Agosti 12,2021 jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la wanawake waombolezao kitaifa amesema kuwa nchi yoyote Duniani ili iweze kuwa na maendeleo ya kukua kiuchumi ni lazima itawaliwe na amani.
Waziri Simbachawene amesema kuwa miradi mbalimbali inayoendelea nchini yote inatokana na utulivu uliotawala baina yetu hivyo serikali inazidi kupata hamasa kuendelea kulijenga taifa kupitia miradi hiyo kuweza kuendeleza mageuzi ya kukua kiuchumi hapa nchini.
Waziri amewasaihi viongozi wa dini kuendelea na maombi hayo ili kuliponya taifa na mambo ambayo siyo mila na utamaduni wa taifa hasa ndoa ya jinsia moja.
Pia amewaomba viongozi hao kuliombea taifa kuwa na amani na utulivu.
“Amani ndiyo msingi wa kila kitu lazima tuendelee kuwekeza katika amani na utulivu badala ya kuwekeza katika madaraja na mambo mengine”aamesema Simbachawene
Hata hivyo amewahakikishia viongozi wa dini kuwa serikali itaendelea kuwezesha wananchi wake kuendelea kuabudu bila kubugudhiwa na mtu yeyote.
“Mnao uhuru wa kuabudu na sisi kama serikali hatuta kuwa kikwazo cha nyinyi kuendelea kuabudu kwa imani zenu bali tutawezesha kwa kuweka sawa mazingira ya kuabudu ila kwa wale ambao watakwenda kinyume na utaratibu basi serikali itashughulika nao”amesema
Mwenyekiti wa kongamano hilo Dk. Juliana Manyerere, amesema kuwa lengo la kongamano ni kuliombea taifa pamoja na mihili yake mitatu.
Dk.Manyerere amessistiza kuwa kutokana na umuhimu wa maombi hayo katika kuliombea taifa hivyo anaiomba serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani kuweza kuendelea kuwaruhusu kufanya makongamano hayo kwaajili ya kuliombea Taifa pindi linapokuwa na misukosuko ya kidunia.
Amesema kuwa kumekuwa na tabia ya watu mbalimbali kuharibu maadili ya Taifa la Tanzania ikiwemo na utoaji Rushwa, Uvaaji mbovu wa mavazi pamoja na ukiukaji wa taratibu na sheria zilizowekwa na serikali ya Tanzania.
"kongamano hili limejengwa kwa mafundisho yatakayo wapatia watu maarifa kuweza kujikwamua katika mahitaji yao pia tunashukuru mafanikio tunayaona japo changamoyo zipo ila tunaomba serikali pia itupe ushirikiano katika kufanikisha makongamano kama haya ya maombi maalumu". amesema Dk.Manyerere
0 Comments