Ticker

6/recent/ticker-posts

WASANII IMARISHENI MASHIRIKISHO YENU-NAIBU WAZIRI GEKUL


**************************** 

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ametoa wito kwa viongozi wa vyama na Shirikisho la Muziki Tanzania (SHIMUTA) kujielekeza katika kuimarisha Shirikisho pamoja na vyama vilivyopo chini ya Shirikisho hilo. 

Mhe. Gekul ameyasema hayo tarehe 18 Agosti, 2021 alipokutana na viongozi wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Vya vilivyo chini ya Shirikisho hilo pamoja na Wasanii Wakongwe wa Muziki wa Dansi jijini Dar es Salaam. 

"Wekezeni nguvu kubwa katika kuimarisha uongozi na utendaji wa Shirikisho pamoja na Vyama vyenu ili kuondoa migogoro ya mara kwa mara inayorudisha nyuma maendeleo ya wanachama wenu" - amesema Gekul. 

"Kumekuwa na migogoro mingi kwenye mashirikisho jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya Sekta ya Sanaa hususani Tasnia ya Muziki hapa nchini" - ameeleza Gekul. 

Mhe. Gekul pia alielekeza Basata kufanya kazi kwa karibu na viongozi wa Shirikisho la Muziki Tanzania ikiwa ni pamoja na kufuatilia kwa karibu uendeshaji wa shughuli zao za kila siku pamoja na kuhakikisha viongozi wanafuata katiba ya Shirikisho. 

"Uongozi wa Shirikisho upo madarakani kwa zaidi ya siku tisini sasa na hawajakutana na kufanya vikao kama katiba yao inavyowatala, huu ni ukiukwaji wa Katiba na unawawinya wanachama haki yao ya msingi ya Kikatiba" alisisitiza Gekul. 

Katika kikao na Wasanii wakongwe wa Muziki wa Dansi, wasanii witoa maombi mbalimbali kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kilio cha wizi wa kazi zao pamoja na mapato kidogo ya mirabaha. 

"Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kwa dhati kulinda haki za wasanii pamoja na kuongeza kipato kupitia kazi zao hususani kazi za muziki ambapo kwa sasa tupo kwenye hatua za mwisho za maboresho ya kanuni ili kukusanya kodi ya vifaa vya kuhifadhi na kusambaza kazi za muziki kabla havijaingia sokoni ( Blanc Tapelevy) na kutoa gawio la0 mapato hayo kwa wasanii" - amesema Gekul 

Aidha, Naibu Waziri Gekul aliwaagiza COSOTA kukamilisha kwa haraka mfumo wa kieletroniki wa kukusanya mirabaha ya wasanii. 

Wasanii wakongwe mbalimbali walishiriki katika kikao hicho kama vile Mzee Ally Zoro, Mwijuma Muumini, Luiza Mbutu, Juma Kelele, Kalala Junior na wengine wengi ambapo waliishukuru Serikali kwa kuwekeza mipango madhubuti ya kutatua changamoto za wasanii nchini.

Post a Comment

0 Comments